Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni
Mchome (kushoto) akiongozana na wadau wengine wa Mahakama ya Tanzania
walipotembelea kuangalia Maandalizi ya Jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama
ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililopo kwenye Shule ya Sheria Sinza leo
jijini Dar es salaam. Baadhi ya Wadau wa Mahakama waliotembelea Mahakama hiyo
ni Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Wizara ya
Mawasiliano, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka
(DPP), na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)
Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania,
Hussein Kattanga (kulia) akiwaelezea jambo baadhi ya Makatibu Wakuu na
watendaji wakuu wa Wizara na Taasisi za Serikali ambao ni Wadau wa Mahakama ya
Tanzania walipotembelea kuona maendeleo ya Maandalizi ya Jengo litakalotumika
kuwa Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Sinza jijini Dar es
salaam. Anayetazamana na Kattanga ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria
Prof. Sifuni Mchome na anayefuatia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Ufundi Bibi Maimuna Tarishi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni
Mchome (kushoto) na Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga
(kulia) wakiwaonyesha jambo wadau wengine wa Mahakama walipotembelea jengo
litakalotumika kuanzisha Mahakama ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo
jijini Dar esa salaam
Makamu
Mkuu wa Shule ya Sheria (Fedha na Utawala) Dkt. William Pallangyo na Mtendaji
Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Hussein Kattanga wakielezea jambo kwa wadau wa
Mahakama ya Tanzania walipotembelea jengo litakalotumika kuanzisha Mahakama ya
Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi lililopo Sinza jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment