Balozi
wa Palestina nchini Tanzania Bw. Hafen Shabit akisoma dua mara baada ya kutia
saini kitabu cha maombolezo kilichopo katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa
Luthuli, jijini Dar es Salaam.
Balozi
wa Uganda nchini Tanzania Bi. Dorothy Samali Hyuha akisaini kitabu cha
maombolezo na kutoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha aliyekua Rais wa
Pili wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mzee Aboud Jumbe Mwinyi.
Mwakilishi
wa Ubalozi wa Nigeria nchini Bi. Abiola Sherif Deluya akitoa salamu za pole
katika kitabu maalumu kilichopo katika Ofisi ya Makamu wa Rais Mtaa wa Luthuli,
Jijini Dar es Salaam leo.
Balozi
wa Kuwait nchini Tanzania Bw. Jassem Al
Najem ni miongoni mwa mabalozi waliotembelea Ofisi ya Makamu wa Rais leo na
kutoa salamu za pole kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wa Awamu ya Pili wa
Zanzibar. Picha
zote na Ofisi ya Makamu wa Rais
No comments:
Post a Comment