*Awapongeza kwa Uzalendo wao Kwa Taifa letu .
*Awaahidi kuwapatia Ambulance
*Awataka Waifanye Dar Kama Dubai Kiulinzi.
Na Mwandishi wetu Dar
Mkuu wa Mkoa wa Dar Mh.Paul Makonda Leo amekutana na kikosi cha kutuliza ghasia (FFU) Ukonga Jijini Dar es Salaam na kuzungumza nao kuhusu suala zima la ulinzi.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Makonda aliwapongeza askari hao kwa uzalendo wao wa kulitumikia Taifa, ambao wapo tayari kufa kwa ajili ya Taifa letu Liwe salama.
Aidha Rc Makonda amewataka Askari hao kuendelea kuimarisha ulinzi ili kufikia malengo na kufikia viwango vya nchi kama Dubai.
Mh. Makonda amewaahidi askari hao wa FFU Ukonga kuwapatia gari la wagonjwa ili liwasaidie askari katika hospitali yao huku akiahidi kufuatilia ombi lake alilolitoa siku ya uzinduzi wa huduma ya polisi kwa wananchi pale viwanja vya Biafra mbele ya Mhe Rais Dkt.John Magufuli.
Makonda alitoa ahadi ya kufuatili kuhusu asilimia 20% ya faini zinazotozwa na askari wa Usalama Barabarani zibaki kwa askari ili kuboresha utendaji ikiwa ni pamoja na ukarabati wa Magari ya askari sambamba na mafuta ili polisi watakapohitajika wawe wanafika bila kuchelewa
Mhe. Makonda akizungumza na baadhi ya Askari
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mhe. Paul Makonda, akizungumza katika hafla hiyo.

Mkuu wa Mkoa katika hafla hiyo.




No comments:
Post a Comment