Habari za Punde

*PSPF YAONGEZA WANACHAMA KUPITIA MPANGO WA PSS KWENYE MAONYESHO YA AIRTEL BAZAAR JIJINI DAR

Mkuu wa Kitengo cha Usajili Wanachama Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw.Msafiri S. Mugaka, akimkabidhi Bw. Kenny Rodgers, kadi ya uanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa uchangiaji wa hiari,(PSS), wakati wa maonyesho yaliyoandaliwa na kampuni ya simu za mikononi, Airtel, yaliyopewa jina la Airtel Bazaar yaliyolenga kuwakutanisha wateja wa kampuni hiyo na kampuni nyinhione zinazotoa huduma na kufanyika makao makuu ya Airtel, Morocco jijini Dar es Salaam, Agosti 12, 2016. PICHA NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
Bw. Kennedy akijaza fomu tayari kujiunga na mpango wa PSS wa PSPF
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Maseka Kadala, (kulia), akipatia maelezo, mfanyakazi wa Airtel alipotembeela banda la Mfuko huo. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE
Mfanyakazi huyu wa Airte, akisoma kipeperushi kabla ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, PSS
Hadji Jamadari, Afisa Mkuu wa Matekeelzo wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, akimkabidhi kadi ya kujiunga na uanachama wa Mfuko huo kupitia PSS, Bw.Anthony S. Masha, baada ya kujiunga.
Afisa Matekelezo msaidizi wa PSPF, Penzila Kaisi, akimpatia maelezo juu ya huduma mbalimbali ambazo Mfuko unatoa, kwa mwanachama
Herman F. Laswai, (kushoto), akikabidhiwa kadi yake ya kujiunga na uanachama wa PSPF, kupitia Mpango wa uchangiaji wa hiari, (PSS), kutoka kwa Afisa Matekelezo msaidizi wa Mfuko huo, Angelina Kombe
Angelina Kombe, Afisa Matekeelzo Msaidizi wa PSPF, akimpatia maelezo kwa umakini mkubwa mwananchi huyu aliyetembelea banda la PSPF
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Maseka Kadala, (kulia), akimsikilzia kwa makini mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo ambapo baadaye alijiunga baada ya kuelewa huduma za Mfuko huo.
Wananchi wakipatiwa huduma na maafisa wa PSPF.
Elimu ikiendelea kutolewa kuhusu huduma za Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kwa wananchi waliotembelea banda la Mfuko huo.
Penzila Kaisi (kulia), Afisa Matekelezo msaidizi wa PSPF, akimuelimisha mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo ili kujua shughuli zake
Mkuu wa kitengo cha kuandikisha wanachama cha Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Msafiri S. Mugaka, akiwapatia maelezo wanachama hawa wa PSPF, kuhusu mafao na faida nyingi ambazo mwanachama anaweza kupata ikiwa ni sehemu ya huduma zitolewazo na Mfuko.
Angelina akitoa somo kwa mwananchi huyu.
Afisa Matekelezo wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Maseka Kadala, (kulia), akimsikilzia kwa makini mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo ambapo baadaye alijiunga baada ya kuelewa huduma za Mfuko huo.
Mkuu wa kitengo cha kuandikisha wanachama cha Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Msafiri S. Mugaka, akiwapatia maelezo wanachama hawa wa PSPF, kuhusu mafao na faida nyingi ambazo mwanachama anaweza kupata ikiwa ni sehemu ya huduma zitolewazo na Mfuko.
Mwanachama mpya akijaza fomu za kujiunga na mpango wa PSS
***************************************
Na Khalfan Said
MFUKO wa Pensehni wa PSPF, umeendelea kusajili wanachama wapya kupitia Mpango wa Uchangiaji wa Hiari wa PSS, wakati wa Maonyesho ya taasisi na makampuni ya kutoa huduma yaliyoandaliwa na Kampuni ya simu za mikononi, Airtel na kwenda na jina la Airtel Bazzar na kufanyika makao makuu ya kampuni hiyo Morocco jijini Dar es Salaam, Agosti 12, 2016.
Akizungumza na waandishi wanhabari kwenye banda la Mfuko huo, Mkuu wa Kitengo cha Usajili nwa Wanachama cha Mfuko huo, Bw. Msafiri S. Mugaka, alisema, PSPF kupitia mpango wake wa PSS, imefanikiwa kusajili wanachama wapya kadhaa, ambayo ilikuwa ni moja ya huduma walizokuwa wakizitoa kwenye maonyesho hayo ya siku moja.
"Pia wanachama wetu waliweza kuja na kupatiwa huduma za taarifa za michango yao, wanawezaji kufaidika na mafao mbalimbali ya yatolewayo na Mfuko kama vile fao la Elimu, Uzazi, mikopo kwa wafanyakazi wapya, na mafao mengine kadhaa,"alisema.
Maonyesho hayo yalishirikisha makampuni kadhaa ya kibinafsi na taasisi za umma na yalilenga kuwakutanisha wateja wa Airtel, na taasisi hizo ikiwa ni pamoja na wafanyakazi wenyewe wa Airtel kutembelea taasisi hizo na kupatiwa huduma mbalimbali wakiwa hapo hapo kazini.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.