Habari za Punde

*RASIMU YA TAARIFA YA UTAFITI KUHUSU HALI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA NCHINI YAZINDULIWA LEO JIJINI DAR

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki akizungumza wakati wa uzinduzi wa warsha ya kujadili rasimu ya Taarifa ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini leo Jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo imeratibiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.
 Katibu wa Maadili ya Viongozi – Siasa, Waziri Kipacha  akielezea jambo wakati wa warsha ya kujadili rasimu ya Taarifa ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini leo Jijini Dar es Salaam. Warsha hiyo imeratibiwa na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma.Kutoka kulia ni Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki na Profesa John Kessy kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo (SUA) ambaye ndiye aliyefanikisha utafiti huo.
: Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe. Angela Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Dini pamoja na Vyama vya Siasa nchini  mara baada ya uzinduzi wa warsha ya kujadili rasimu ya Taarifa ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini leo Jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi – CUF Twaha Tasrima, : Kamishina wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Salome Kaganda, Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Phillip Mangula
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Phillip Mangula akiteta jambo na Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi – CUF Twaha Tasrima walipokuta katika warsha ya kujadili Taarifa ya rasimu ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini leo Jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wa warsha ya kujadili Taarifa ya rasimu ya Utafiti kuhusu hali ya maadili ya viongozi wa umma nchini wakifuatilia uwasilishwaji wa rasimu hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Picha na Frank Shija, MAELEZO.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.