Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Mhandisi,Dkt.
Leonard Chiriho akizungumza na
wawakilishi wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China walipotembelea Chuo cha
Taifa Cha Usafirishaji (NIT) jana Jijini Dar es Salaam. Wawakilishi hao
wametembelea chuoni hapo ikiwa ni ziara ya tathmini kama chuo hicho kinakidhi
kupata ufadhiri wa China katika mpango wake wa kujenga Vyuo Vikuu Vitano vya
Usafirishaji Barani Afrika. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi.
Profesa. Zacharia Mganilwa, Katibu wa Tatu Mwakilishi wa Masuala ya Uchumi na
Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Sun Chengfeng, Mwakilishi Mkuu
wa Masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Lin
Zhiyong na Mkurugenzi wa Huduma za Uasafirishaji kutoka Wizara ya Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi. Aron Johnson Kisaka.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Mhandisi,Dkt. Leonard Chiriho akimzungusha Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China Lin Zhiyong (katikati) alipotembelea Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) jana Jijini Dar es Salaam. Mwakilishi huyo alitembelea chuoni hapo ikiwa ni ziara ya tathmini kama chuo hicho kinakidhi kupata ufadhiri wa China katika mpango wake wa kujenga Vyuo Vikuu Vitano vya Usafirishaji Barani Afrika. Kushoto ni Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi, Profesa Zacharia Mganilwa. Picha na Frank Shija, MAELEZO
****************************************************
Na:
Frank Shija, MAELEZO
Chuo
cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kuwa miongoni mwa Vyuo Vikuu Vitano vitakavyo
jikita katika fani za Usafirishaji vitakavyojengwa Barani Afrika kwa msaada wa
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.
Hayo
yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
Mhandisi, Dkt. Leonard Chamuriho alipokutana na Mwakilishi Mkuu wa masuala ya
Uchumi na Biashara kutoka Serikali ya Jamhuri ya Watu wa Chini hapa nchini Bwana
Lin Zhiyong wakati wa ziara ya kufanya tathmini juu ya uwezo wa NIT katika
utoaji wa elimu ya Usafirishaji na namna ya kuweza kukisaidia chuo hicho.
Katika
ziara hiyo Katibu Mkuu huyo amemuhakikishia Mwakilishi Mkuu wa masuala ya
Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuwa NIT iko imara
na inayo mipango kabaambe kwa ajili ya upanuzi wa chuo hicho utakao enda
sambamba na kuongezeka kwa Programs zitakazokuwa zikifundishwa.
“Kutokana
na urafiki wa muda mrefu tulionao baina yetu na China ni imani yangu kuwa Chuo
hiki kitakuwa miongoni mwa Vyuo Vikuu Vitano vya Usafirishaji vitakavyojengwa
kwa masaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China barani Afrika kama ambavyo
Rais wan chi hiyo alivyo dhamiria wakti wa mkutano huko Afrika ya Kusini”
Alisema Dkt. Chamuriho.
Ni
dhahiri kuwa wataalamu wa masuala ya usafirishaji wanatakiwa kwa wingi kwani
ukuaji wa Sekta hiyo unaenda kwa kasi hali kadhali Jiografia ya nchi yetu
inatoa fusra kwa Tanzania kujenga miundombinu ya usafirishaji kama vile Barabara
na miundombinu ya Reli, Viwanja vya Ndege ili kuunganisha na Bandari.
Mpango
huo umekuja katika wakati muafaka kwani utasaidia kuongeza idadi ya waataalam
katika sekta ya usafirishaji kwa kuwa wanafunzi wengi zaidi watajiunga na
masomo mbalimbali yatakayofundishwa katika chuo hicho kitakapo kamilika.
Mhandisi
Profesa Zacharia Mganilwa ni Mkuu wa Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji, anasema
kuwa wao kama uongozi wa chuo wanao mpango mahususi wa kufanya maboresho makubwa
ya Chuo hicho ili kiweze kukidhi mahitaji halisi ya Sekta ya usafirishaji hapa
nchini kwa sasa.
“Sisi
kama Taasisi tumejipanga kuhakikisha tunafanya maboresho ya Chuo chetu ili
kiendane na hali halisi ya ukuaji wa sekta ya usafirishaji hapa nchini, katika
mpango huo tumenuia kuanzisha Shule tano zitakazo jikita katika nyanja za Shule
ya Uhandisi na Teknolojia, Shule ya Teknolojia ya Anga, Shule ya Usafirishaji
na Logistic,Shule ya Elimu, Hisabati na Kompyuta na Shule ya Biashara NIT”.
Mhandisi Mganilwa
Aliongeza
kuwa kutokana na mpango huo NIT inalo maeneo yakutosha na kukidhi mahitaji ya
utekelezaji wa mpango huo kwani ina jumla ya ekari 46 katika eneo la sasa
ambapo kuna ardhi ekari 46 ambapo kati ya hizo ni asilimia 30 tu ndiyo iliyotumika
hadi sasa, pia chuo kimefanya utaratibu wa kupata eneo jingine la ekari 1600
katika wilaya ya Bagamoyo mkoani Pwani.
kizungumza
wakati wa ziara hiyo ya kufanya tathmini ya Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya
Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China nchini Tanzania, Lin
Zhiyong ameonyesha imani kwa Chuo hicho na kuahidi kusaidia katika kuhakikisha
kinakuwa miongoni mwa Vyuo hivyo Vitano vilivyoahidiwa na Rais wao.
Aliongeza
kuwa kutokana na kasi ya maendeleo iliyopo hadi kufikia mwaka 2015 Tanzania
itakuwa nchi ya uchumi wa kati.
“Nimeshawishika
na niliyojionea hapa naweza kusema Serikali yetu itakuwa tayari kusaidia
program mbalimbali zilizopo hapa na kutokana na urafiki wa kihistoria uliopo
nawahakikishia kuwa NIT itakuwa miongoni
mwa Vyuo Vikuu Vitano vya Usafirishaji Barani Afrika vitakavyojengwa na
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kama ambavyo Rais wetu alivyo ahidi wakati
wa Mkutano Jijini Johannesburg, Afrika Kusini”.Alisema Zhiyong.
Zhiyong
aliongeza kuwa ujenzi huo wa Vyuo hivyo unatarajiwa kukamilika ndani ya kipindi
cha miaka mitatu.
Ziara
hiyo ya Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya Uchumi na Biashara wa Serikali ya Jamhuri
ya Watu wa China nchini Tanzania Lin Zhiyong ilikuwa ni kwa ajili ya kufanya
tathmini juu ya program zinazofundishwa, rasilimali watu na miundombinu kwa
maana ya eneo.
No comments:
Post a Comment