Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya,
Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisabisya akiongea na
wadau wa Nchi washiriki kutoka Canada,Uswizi, Denmark na Korea kusini hawapo
pichani wakati wa kusaini msaada wa Bilioni 142.23 kwa ajili ya kuinua vituo
vya afya nchini.
Wadau wa Nchi washiriki kutoka Canada,Uswizi, Denmark na Korea kusini wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisabisya katikati mara baada ya kusaini msaada wa Bilioni 142.23 kwa ajili ya kuinua vituo vya afya nchini. Picha na Ally Daud- Maelezo
******************************************************
Na
Ally Daud-Maelezo
Serikali chini ya Wizara ya Afya,
Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto imepokea msaada wa shilingi bilioni
142.23 kutoka nchi washiriki Canada,
Denmark, Uswizi na Korea Kusini ili kusaidia kuinua vituo vya afya nchini.
Akizungumza mara baada ya kusaini
msaada huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na
Watoto Dkt. Mpoki Ulisabisya amesema kuwa msaada huo wataupeleka moja kwa moja katika
Zahanati za vijiji,Hospitali za Wilaya
na mkoa ikiwa pamoja na vituo vya afya nchi nzima.
“Tumepokea msaada huo kwa furaha kubwa
na kuhaidi kupeleka fedha hizo hizo mahali panapohitajika kwa matumizi ya
kukuza na kuboresha vituo vya afya katika zahanati na hospitali nchi nzima ili
kuokoa maisha ya watanzania” alisema Dkt. Ulisabisya.
Aidha Dkt. Ulisabisya anaishukuru
Benki ya Dunia kwa kuimarisha na kusaidia mfuko wa maendeleo ya afya nchini kwa
kuwakutanisha na wahisani kutoka nchi mbalimbali.
Mbali na hayo Dkt.Ulisabisya amewaomba
Benki ya Dunia na nchi wahisani wasichoke na kushindwa kuisaidia Tanzania
katika sekta ya Afya ili kutokomeza maradhi kwa kiwango kikubwa na kupambana kwa ajili ya kukuza uchumi wan
chi.
No comments:
Post a Comment