Habari za Punde

*YANGA WAKUBALI KUMKABIDHI MANJI TIMU KWA MIAKA 10, AJENGE UWANJA, AWATEMA WAJUMBE WATATU

Na Ripota wa Sufianimafoto Dar
BAADA ya Mwenyekiti wa Yanga Yusuf Manji kuitisha mkutano wa dharula, hatimaye leo, wanachama wa Klabu hiyo wamekubali kumuachia mwenyekiti huyo timu kwa muda wa miaka 10.

Katika Mkutano huo mkuu wa dharula uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam, wanachama wa Yanga kwa pamoja wameridhia na kupitisha suala hilo la kumkabidhi Manji timu na kwa muda huo uliokubaliwa huku akichukua asilimia 
75 ya mapato ya timu na asilimia 25 ikibaki kwa wanachama.

Aidha kwa kipindi cha miaka 10 hiyo, timu ya soka na Nembo ya Klabu vyote vitamilikiwa na Manji. 

Akizungumza katika mkutano huo,  Mjumbe wa Baraza la Wadhamini la klabu, hiyo, Francis Kifukwe, alisema kuwa kutokana na wanachama kuridhia kwa pamoja maamuzi hayo, na wao kama Baraza la Wadhamini wanamkabidhi madaraka hayo Manji.

Naye Manji akizungumza katika mkutano huo baadaya kukabidhiwa rasmi, aliwataka wanachama kumwamini na kuwataka waridhie kuteua Wajumbe wa kufanya nao kazi, ambapo aliwataja baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya utendaji kama Salum Mkemi, Ayoub Nyenzi na Hashim Abdallah, kuwa awahitaji katika orodha ya wajumbe anaohitaji kufanya nao kazi, ambapo waliondolewa katika mkutano huo. 
Kwa kutumia Demokrasia Mwenyekiti Manji aliwahoji wanachama hao kuwa iwapo kuna anayewahitaji wajumbe hao, basi anyooshe mkono ili wapigiwe kura jambo ambalo alikufanyika kutokana na wanachama wote kutojitokeza kwa hilo.

Kati ya wanachama hao waliotajwa ni Abdallah pekee aliyekuwepo ukumbini humo na kutoka nje, huku Siza Lyimo akisimama na kuomba msamaha kwa wanachama na Mwenyekiti kuamua kumsamehe na kufanya mkutano huo kuendelea hadi kumalizika kwa amani.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.