Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe.
George Boniphace Simbachawene akizungumza wakati wa mkutano baina yake na
wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Ofisini kwake leo Jijini Dar es
Salaam kwa lengo la kuwasilisha taarifa ya tathimini ya utekelezaji wa Mpango
wa Urasimishaji wa Rasilimali na Biashara katika Halmashauri nchini.Kushoto ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniphace Simbachawene akizungumza wakati wa mkutano baina yake na wajumbe wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Ofisini kwake leo Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwasilisha taarifa ya tathimini ya utekelezaji wa Mpango wa Urasimishaji wa Rasilimali na Biashara katika Halmashauri nchini.Kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa Mkurabita Kapteni Mstaafu John Chiligati.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Uongozi wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara Tanzania
(MKURABITA) Mhe. Kapteni Mstaafu John Chiligati akielezea jambo wakati wa kikao
baina ya kamati hiyo na TAMISEMI kuhusu tathmini ya utekelezaji wa mpango huo
katika Halmashauri mbalimbali nchini leo Jijini Dar es Salaam. Kutoka Kulia ni
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Mhe. George Boniphace Simbachawene, Mratibu wa MKURABITA Bibi. Seraphia Mgembe
na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA Profesa. Aldo Lupala.
****************************************************************
Na:
Frank Shija – MAELEZO.
Kufuatia
kusuasua kwa utekelezaji na maendeleo ya Mpango wa Urasimishaji wa Rasilimali
na Biashara Serikali imeziagiza Halmashauri zote nchini ambazo zimefikia na
mpango huo kuwasilisha taarifa rasmi.
Agizo
hilo limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa Mhe. George Boniphace Simbachawene katika kikao baina yake na wajumbe
wa Kamati ya Uongozi wa MKURABITA kilichofanyika Ofisini kwake leo Jijini Dar
es Salaam.
Simbachawene
amesema kuwa TAMISEMI ni mdau muhimu katika Mpango huo wa urasimishaji wa
rasilimali hivyo ujio wa kamati hiyo kutaka kushirikiana na Tawala za Mikoa ni
jambo jema.
“Binafsi
ni muumini wa muda mrefu wa mpango huu wa urasimishaji, niseme tu mmechelewa
kuja sehemu husika kwa bila dhana ya ugatuaji wa madaraka kwa wananchi
kufanikiwa kwa mpango huu itakuwa ni adithi sasa tutaenda pamoja ili kiutimiza
azma ya mpango huu,”alisema Simbachawene.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya MKURABITA Kapteni wa Jeshi
Mstaafu John Chiligati amesema kuwa pamoja na kuwepo kwa Halmashauri zaidi ya
100 nchini mpaka sasa utekelezaji wa mpango huo umezifikia takribani
Halmashauri 52 na Miji 9 tu hivyo kasi yake bado hairidhishi.
Aliongeza
kuwa changamoto wanazokumbana nazo katika utekelezaji wa mpango huo ni
Halmashauri kuuona mpango huo kama hawahusiki nao hali inayopelekea kushindwa
kuendelea pindi mwakilishi wa Mkurabita atakapo ondoka katika eneo husika.
Chiligati
amesema kuwa baada ya kubaini changamoto hiyo waliamua kuwa na makubaliano
maalum na TAMISEMI juu ya utekelezaji wa pamoja wa mpango huo jambo ambalo
wanaendelea kulifanyia kazi.



No comments:
Post a Comment