Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina
akiangalia suruali aina ya Jinsi
zinazozalishwa katika kiwanda cha EPZ wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa
mazingira mapema hii leo Jijini Dar es salaam.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina
akiwa katika ziara ya ukaguzi wa Mazingira katika kiwanda cha uwekezaji cha
EPZ, kilichopo Terminal Jijini Dar es salaam. 
. Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Luhaga Mpina
akiangalia shughuli za uzalishaji wa nguo katika kiwanda cha nguo cha EPZ mara
baada ya kufanya ziara ya ukaguzi wa mazingira katika kiwanda hicho kilichopo
Ubungo Terminal Jijini Dar es salaam.
****************************************************
SERIKALI imetoa siku 30 kwa Kiwanda cha KOBIL kilichopo
maeneo ya Keko kuvunja jengo lake lililojengwa juu ya mtaro wa
kupitishia maji ya mvua na kusababisha maji hayo kutopita
vizuri.
Akitoa agizo hilo Jijini Dar es Salaam, Naibu Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais- Mazingira na Muungano,Luhaga Mpina
amesema mnamo Februari 15 mwaka huu,alifanya ukaguzi katika
eneo la Keko na kutoa maelekezo kwa kiwanda cha Kobil kumpatia
taarifa juu ya nyaraka zao zilizowahararishia kujenga jengo
lao juu ya mtaro huo.
Amesema alipitia taarifa za kiwanda hicho cha kobil Tanzania
na kujiridhisha nayo kuwa hakuna kibari chochote kilichotolewa
dhidi ya kiwanda hicho kujenga juu ya mtaro huo.
Mpina amesema kujenga jengo juu ya mtaro au mfereji wa maji ya
mvua ni kinyume cha sheria ya Mazingira namba 20 ya mwaka
2004,Sheria ya ardhi namba 4 ya mwaka 1999 ambapo pia ni
kinyume cha sheria ya mpango mji ya mwaka 2007.
"Februari 15 mwaka huu,nilifanya ukaguzi katika eneo la Keko
ambapo baadhi ya viwanda viwili vilijengwa juu ya mtaro wa
maji ya mvua na kusababisha kero kwa wananchi wa eneo hilo
pale mvua zinaponyesha,hivyo nilitoa agizo ya kiwanda cha
Redsea kubomoa jengo lake ndani ya siku 30 na leo natoa agizo
kwa Kobil kubomoa jengo lao ndani ya siku hizo,"amesema
Aidha amesema kuwa Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC)
liwaandikie hati ya siku 30 Kampuni hiyo ya Kobil kubomoa
wenyewe jengo lao na endapo hawatabomoa serikali itabomoa kwa
gharama zao wenyewe.
Mpina ameseama viwanda hivyo vimejengwa juu ya mtaro ambapo
mvua kubwa ikinyesha maji ya mvua hayo yanashindwa kupita
vizuri na kusababisha mafuriko makubwa kwa wananchi.
Ameongeza kuwa Kobil inatakiwa kubomoa jengo lao ili kupisha
mfereji huo wa maji ya mvua kuongeza kasi ya maji ya mvua
pindi mvua inaponyeshwa.
"Tumejiridhisha vya kutosha kwamba hakuna upepembuzi yakinifu
uliofanyika katika majengo haya wakati wa majengo haya
yalipokuwa yanajengwa,"amesema Mpina.
No comments:
Post a Comment