Meneja
Mauzo na Masoko wa Kampuni ya magazeti ya serikali (TSN), Bw. Januarius
Maganga (kulia) akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Mamlaka ya
Viwanja vya ndege Tanzania (TAA), kwenye maonesho ya washiriki wa
Kongamano la Mazingira la wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria
linalofanyika Mwanza. Kushoto ni Mhandisi Diana Munubi wa TAA.
Raia wa
Kenya, John Osodo (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Diana
Munubi (kulia) alipotembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), kwenye maonesho ya Washiriki wa Kongamano la Mazingira la
Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria linalofanyika Jijini
Mwanza.

Dkt.
Frank Mgeta wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza, Sekou-Toure (kulia),
akipata maelezo mbalimbali yanayohusu mazingira kutoka kwa Mhandisi Diana
Munubi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), kwenye maonesho ya
washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la
Ziwa Victoria, jijini Mwanza.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dkt
Leonard Chamuriho (kushoto) akisalimiana na Meneja wa Kiwanja cha Ndege
cha Mwanza, Bi. Esther Madale kwenye banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege
Tanzania (TAA), katika maonesho ya
Washiriki wa Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la
Ziwa Victoria linalofanyika jijini Mwanza.
Katibu
Mkuu, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya Uchukuzi), Dkt
Leornard Chamurho (kushoto), akifurahia maelezo yanayotolewa na Meneja wa
Kiwanja cha Ndege cha Mwanza, Bi. Esther Madale kwenye banda la Mamlaka ya
Viwanja vya ndege Tanzania (TAA), katika maonesho ya Washiriki wa
Kongamano la Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria linalofanyika
jijini Mwanza.
Mhandisi
Diana Munubi (wa kwanza kulia) akitoa maelezo yaliyomfurahisha Katibu Mkuu
wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi), Dtk.
Leonard Chamurho (wa kwanza kushoto), akifuatiwa na Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamu wa Rais, Prof. Faustine Kamuzora, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maji
na Umwagiliaji, Mhandisi Emmanuel Kalobelo na Afisa Usafirishaji Mkuu wa
Uchukuzi, Alphonce Mwingira katika maonesho ya Washiriki wa Kongamano la
Mazingira la Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria linalofanyika
jijini Mwanza.
Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi) kutoka taasisi za TAA, TCAA, TMA na DMI
wanaoshiriki kwenye maonesho ya washiriki wa Kongamano la Mazingira la
Wanasayansi Watafiti wa Bonde la Ziwa Victoria, linalofanyika Mwanza, wakiwa
kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu Uchukuzi, Dkt. Leonard Chamurho, Katibu
Mkuu Ofisi ya Rais, Prof. Faustine Kamuzora, na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya
Maji na Umwagiliaji Mhandisi Emmanuel Kalobelo.





No comments:
Post a Comment