Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz akimtambulisha Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa wafanyakazi wa alipofanya ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.

Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa akimwelezea jambo Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa wafanyakazi wa alipofanya ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwasili katika Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Kampuni za Bakhresa Bw. Salim Aziz.
Rais wa Uganda Mhe.Yoweri Museveni(wapili kushoto) akiulizia jambo wakati wa ziara yake katika viwanda vya Kuzalisha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Hussein Sufiani na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Baadhi ya wafanyakazi wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa wakifurahia ugeni wa Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni(hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika viwanda vya Kuzalisha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam leo.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz akimkabidhi zawadi Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akifurahia zawadi aliyopewa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (wapili kulia) mara baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akishukuru kwa kupewa zawadi ya maboksi ya Juisi za Azam mara baada ya kumaliza ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (kulia).
Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akishukuru kwa kupewa zawadi ya maboksi ya Juisi za Azam mara baada ya kumaliza ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (kulia).
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Ziara ya Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz.
Mkurugenzi wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa akifafanua jambo
mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Ziara ya Rais wa
Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa Ngano
Cha Bakhresa Food Products kilichopo
Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti
Jijini Dar es Salaam leo.
Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni(mweneye kofia) akiwa katika picha ya pamoja na menejimenti ya Kundi la Makampuni ya Bakhresa mara baada ya kumaliza ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.
Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.
*****************************************************************
Na.
Immaculate Makilika na Lilian Lundo- MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe.
Yoweri Museveni ametoa wito wafanyabiashara wa Kitanzania kwenda kuwekeza
nchini Uganda.
Rais Museveni ametoa kauli hiyo leo
wakati alipotembelea viwanda vya Kampuni ya Bakhresa vinavyozalisha Unga
na Juisi vya Buguruni na Vingunguti jijini Dar es Salaam.
“Nawakaribisha
wafanyabiashara wa Kitanzania kuja nchini Uganda kuwekeza kwani kufanya hivyo
kutasaidia kuzalisha bidhaa, upatikanaji wa soko pamoja na ajira” alisema Rais
Museveni.
Kauli hiyo ya Rais Museveni
imetokana na mafanikio yanayotokana na Mwekezaji wa Kitanzania Said Salim
Bakhresa aliyewekeza nchini Uganda ambapo anamiliki Kiwanda cha kusanga ngano
nchini humo.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa
Mahusiano wa Kampuni za Bakhresa Hussin Sufiani amesema kwamba Kampuni hiyo iko
mbioni kuongeza uzalishaji wa unga wa ngano kutoka tani 1,100 hadi kufikia tani
2,000 kwa siku nchini Uganda.
Aidha, amesema kutokana na
uwekezaji wa Kampuni hiyo nchini Uganda jumla ya Waganda 650 wamenufaika na
ajira mbalimbali ambazo zinasaidia kuwapatia kipato.
Kwa upande wa Waziri wa Viwanda,
Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwaijage amesema kuwa Uganda na Tanzania
zimeingia makubakliano ya ushirikiano katika sekta mbalimbali
ikiwemo sekta ya viwanda.
Amesisitiza Watanzania wanaweza
kwenda kuwekeza nchini Uganda kwa vile nchi hiyo wanalima tani milioni 4 za
mahindi lakini wana uwezo wa kutumia tani milioni moja pekee, hivyo ni fursa
kwa wafanyabiashara wa Kitanzania kwenda kuwekeza nchini humo.
“Tunawahamasisha wafanyabiashara wa
Uganda na Tanzania kuwekeza katika nchi zao ili kuzalisha , bidhaa na ajira za
kutosha kwa wananchi” alisema Waziri Mwijage.
Waziri Mwijage alitoa Wito kwa
Watanzania kushiriki katika uchumi wa viwanda kwa kufanya uzalishaji wa bidhaa
zinazotumika viwanda mfanio kwa kulima matunda au mbogamboga.
Rais Yoweri Museveni aliwasili
nchini jana kwa ziara ya kiserikali ya siku mbili ambapo akiwa nchini alifanya
mazungumzo na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt.
John Pombe Magufuli na kutembelea Viwanda vya Said Salim Bakhresa vya
Tazara na Vingunguti.











No comments:
Post a Comment