Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, Januari Makamba
(katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa agizo la
kupiga marufuku uzalishaji na uuzaji wa pombe aina ya viroba leo Jijini Dar es
Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na
Muungano Profesa Faustine Kamuzora na Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi hiyo
Richard Muyungi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, Januari Makamba (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa agizo la kupiga marufuku uzalishaji na uuzaji wa pombe aina ya viroba leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano Profesa Faustine Kamuzora na Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi hiyo Richard Muyungi.
*********************************************************************
Na:
Frank Shija - MAELEZO
SERIKALI
imepiga rasmi marufuku matumizi ya pombe zinazofungashwa katika vifungashio vya
plastiki maarufu kama viroba kuanzia tarehe 1 Machi 2017.
Hayo
yamebainishwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano
Januari Makamba wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es
Salaam.
“Dhamira
ya Serikali siyo kupiga marufuku vinywaji vya pombe kali bali ni kutekeleza
Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ambayo inatoa
haki ya kuishi katika mazingira yaliyo safi, salama na yenye afya,” alisema
Makamba.
Aliongeza
kuwa uamuzi huo wakusitisha matumizi ya pombe hizo, Serikali itatumia Sheria ya
Mazingira ya mwaka 2004 ambapo alitumia fursa hiyo kutangaza utaratibu wa
utekelezaji wa maamuzi hayo.
Alizitaja
taratibu hizo kuwa ni pamoja na kutungwa kwa kanuni zitakazodhibiti uzalishaji
wa vifungashio vya plastiki kwa mujibu wa kifungu 230 (2) (F) CHA Sheria ya
mazingira ya 2004.
Aidha
Waziri Makamba ametoa wito kwa wazalishaji wa pombe kali wanaohitaji muda wa
ziada wa kuhamia katika teknolojia ya chupa kuwasilisha maombi yao kwa ajili ya
kupewa kibali cha kuendelea na uzalishaji huku wakihama kabla ya tarehe 28
Februari.
Makamba
alisema kuwa maombi hayo yaambatanishwe pamoja na ushahidi wa barua ikionyesha
mwenendo wa ulipaji wa kodi, nyaraka kutoka Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA)
kuhusu usalama wa kinywaji, uthibitisho wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS),cheti
cha tathmini ya athari za mazingira, uthibitisho kuwa atatumia teknolojia ya
kudhibiti utengenezaji wa vifungashio bandia na uthibitisho kutoka Wakala wa
Usajili wa Biashara na Leseni.
Katika
hatua nyingine Waziri Makamba amewaagiza Wakuu wa Wilaya nchini kuendesha
operesheni kwa ajili ya kudhibiti uingizwaji wa pombe kali zinazotoka nje na
kuzuia matumizi ya pombe haramu aina ya Gongo.
Utekelezaji
wa uamuzi huo unafuatia dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kusitisha
matumizi ya vifungashio vya plastiki ikiwemo pombe za viroba iliyotolewa bunge
mwezi Mei 2016, Agosti na Desemba 2016 na kufuatiwa na agizo la Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa Majaliwa akiwa ziarani mkoani Manyara aliagiza kusitishwa kwa
utengenezaji, uuzaji na matumizi ya pombe zunazofungashwa kwenye vifungashio
vya plastiki kuanzia tarehe 1 Machi.


No comments:
Post a Comment