SIMBA leo imerejea tena kileleni mwa Ligi Kuu Bara baada ya kuibuka na ushindi mnono wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba sasa wanafikisha jumla ya pointi 51 na kuwaengua kileleni watanani zao wa Jadi Yanga waliokuwa wakiongoza Ligi hiyo kwa tofauti ya pointi 1 wakiwa na Pointi 49.
Dakika 10 baadae Simba waliandika bao la pili kupitia kwa Ibrahim Ajibu akiunganisha krosi ya Loudit Mavugo.
Simba waliandika bao la tatu kupitia kwa Loudit Mavugo kwa kichwa akiunganisha krosi ya Ajibu.
Simba: Daniel Agyei,Method Mwanjale/Mwinyi Kazimoto, Javier Bukungu, Mohamef Hussein, Novalty Lufunga, Said Ndemla, James Kotei, Mzamiru Yassin, Ibrahim Ajibu/Pastor Athanas, Laudit Mavugo na Juma Luizio/Shiza Kichuya.
Prisons: Laurian Mpalile, Aron kalambo, Salum Kimenya, James Mwasote, Nurdin Chona, Jumanne Elifadhili, Lambart Sabiyanka, Kazungu Nchinjayi/Kassim Hamis, Victor Hangaya, Mohamed Samata na Benjamin Asukile/Meshaki Selemani.
No comments:
Post a Comment