Msemaji wa chama cha Maafisa Mawasilino
Serikalini (TAGCO) Bw. Abel Ngapemba (wa
pili kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Tamasha la kufanya mazoezi, kupima afya,kuchangia damu,leo
jijini Dar es Salaam katika ulioshirikisha
Jukwaa la Wahariri (TEF) pamoja na Klabu ya Waandishi wa Habari Dar es Salaam. Tamasha
hilo litafanyika siku ya Jumamosi katika
Viwanja vya Mnazi Mmoja Kuotoka kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa, Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Theophil na Katibu wa Klabu ya waandishi wa
habari Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Siyovera Hussein.
Mkurugenzi
Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa (wa kwanza kulia) akitoa
wito kwa wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kujitokeza kwa wingi kushiriki
katika Tamasha la Mazoezi ambalo litawapa wananchi fursa ya kufanya mazoezi na kupima afya bure kuitikia wito wa Makamu
wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan.Wengine ni wajumbe wa Kamati ya Maandalizi ya
Tamasha hilo.
Katibu wa Klabu ya waandishi wa habari Mkoa wa Dar es Salaam Bw.Siyovera Hussein akisisitiza jambo kwa waandishi wa Habari (hawapo pichani) leo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano uliolenga kuhamasisha wananchi kushiriki katika Tamasha linalolenga kuwahamasisha wananchi kufanya mazoezi . Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Theophil Makunga
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF) Bw. Theophil Makunga akizungumza wakati wa mkutano huo leo Jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa waandishi wa habari kushiriki katika tamasha hilo. Kutoka kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa na Msemaji wa chama cha Maafisa Mawasilino Serikalini (TAGCO) Bw. Abel Ngapemba
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo Leo Jijini Dar es Salaam. Picha na: Frank Mvungi - Maelezo
No comments:
Post a Comment