Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano
na Mazingira Mh. January Makamba akiangalia bonde la mtop Msimbazi katika kata
ya Vingunguti lilivyoharibika kwa shughuli za kila siku za Wananchi ikiwemo
kilimo cha mbogamboga na uchimbaji wa mchanga. Waziri Mkamba yupo katika ziara
kutembelea kata ya Vingunguti kukagua athari za mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba pamoja na Mbunge wa jimbo la Segerea Mh. Bonnah Klauwa wakiskiliza kero mbalimbali zinazotolewa ana Wananchi wakati Mh. Waziri alipofanya ziara katika kata ya Vingunguti kukagua athari mbalimbali za mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea na Wananchi waliojikusanya kumsikiliza wakati wa ziara yake katika kata ya Vingunguti katika wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akipata maelezo, toka kwa vijana wa kata ya Vingunguti juu ya utenegenezaji wa majiko ya mkaa ambayo ni rafiki wa mazingira na ambayo hayatumii mkaa mwingi. Habari na picha toka Kitengo caha mawasiliano Serikalini OMR
*******************************************************
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Rais-Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amewataka wachimbaji mchanga na walimaji
wa bustani katika bonde la mto msimbazi katika kata vingunguti iliyopo katika
Manispaa ya Ilala, kuondoka mara moja na kuacha shughuli hizo. Ameyasema hayo
alipokua katika ziara ya siku moja ya kutembelea kata ya Vingunguti na kujionea
athari mbalimbali za kimazingira katika kata hiyo.
Wakiongea mbele ya Waziri Makamba, Wananchi
wamelalamika kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo bonde hilo kuzidi kumong'onyoka
na kusogelea makazi ya watu pamoja na eneo la makaburi. Hivyo basi kusababisha
nyumba zao kuanguka na makaburi kumong'onyoka hali amabayo inahatrisha maisha
yao na kuwafanya kuishi kwa hofu.
Akijibu kero hiyo Waziri Makamba aliwaambia
kuwa atayafanyia kazi maombi yao na atakaa na viongozi wa Manispaa na wa Ofisi
yake ili kupata suluhu ya matatizo yao. Pamoja na hayo alisema kuwa kwa hatua
za awali anawataka wachimbaji na
wakulima wa bustani kuacha mara moja shughuli hizo wanazofanya katika maeneno
ya bonde hilo.
No comments:
Post a Comment