Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na
Mipango Doto James akizungumza na Wanahabari kuhusu Wizara yake ilivyotekeleza
Agizo la Rais Dkt. John Magufu kuhusu
kumlipa Mkandarasi ayejenga Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere (Terminal 3).
*****************************************
Katika Hatua nyingine Wizara ya Fedha inaandaa
Malipo ya awali (Advance Payment) kiasi cha Tsh. Bilioni 300 kwa ajili ya
kumlipa Mkandarasi anayejenga Mradi wa Ujenzi wa Reli ya Kisasa ya Kutumia
Umeme na Mafuta(Standard Gauge) katika awamu ya kwanza itakayoanzia kutoka Dar
es Salaam hadi Morogoro katika awamu yake ya kwanza ya Ujenzi huo.
*****************************************
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu Doto
James, Wizara ya Fedha na Mipango imemlipa Mkandarasi anayejenga Mradi wa upanuzi
wa wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(Terminal 3) Kampuni ya BAM
International kiasi cha Euro Milioni 9.5 sawa na zaidi ya Tsh. Bilioni 22 za Kitanzania mara baada ya
kuhakiki madai hayo.

No comments:
Post a Comment