Mtambo wa
kudhibiti vumbi katika kiwanda cha saruji cha Moshi ambao haufanyi kazi
ipasavyo, kumekua na malalamiko kutoka kwa wananchi juu ya uchavuzi wa hewa
ufanywao na kiwanda hicho. Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
NEMC Kanda ya Kaskazini ilitoa maelekezo ambayo hayakutekelezwa
kikamilifu, hivyo kiwanda hicho
kimefungwa hii leo.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba alipotembelea
kiwanda cha saruji cha Moshi. Kiwanda hicho kimefungiwa baada ya kutotekeleza
maagizo waliyopewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC). Katikati ni Mwakilishi wa Kiwanda hicho Bi. Sophia na kushoto ni Dkt.
Menan Jangu kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira Kanda
ya Kaskazini.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akisalimiana
na Mkuu wa Wilaya ya Rombo Bi. Agness Hokororo mara baada ya kuwasili wilayani
hapo kwa ziara ya kikazi.
****************************************************************
Ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya
Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. January Makamba hii leo ametembelea
Mkoani Kilimanjaro katika Wilaya ya Rombo. Akiwa Wilayani hapo Waziri Makamba
ametembelea Kiwanda cha Saruji cha Moshi kufuatia malalamiko ya wananchi juu ya
uchafuzi wa hewa itokanayo na vumbi katika shughuli za uzalishaji.
Akitoa maelezo wa awali, Mkuu wa
Wilaya ya Rombo Bi. Agness Hokororo amesema kuwa Kiwanda hicho kimeendesha
shughuli za uzalishaji wa sementi kwa kutofuata sheria ya mazingira ya mwaka
2004 ikiwa ni pamoja na kutokuwa na mfumo mzuri wa kudhibiti uchafuzi wa vumbi
kiwandani hapo.
kwa upande mwingine Dkt. Menan Jangu
Mratibu wa Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa
Mazingira Kanda ya Kaskazini amesema kuwa Ofisi yake awali ilitembelea kiwanda
hicho na kutoa muongozo na taratibu zinazotokiwa kufuatwa kwa mujibu wa Sheria
ya Mazingira ya mwaka 2004.
"Tuliwaelekeza kufanya
yafuatayo, kujenga fensi kuzunguka eneo lote la kiwanda, kujenga
"pevements" na kuweka mashine maalumu ya kuzuia vumbi kusambaa kwa
wingi angani, vitu ambavyo havijafanyiwa kazi." Alisisitiza Dkt. Jangu
Mwakilishi wa Kiwanda hicho raia wa
China aliyefahamika kwa jina moja tu Bi. Sophia, amesema kuwa suala la kuzungusha
uzio eneo lote litatekelezwa pindi hati miliki ya ardhi ya eneo hilo
itakapopatikana.
Waziri Makamba aliagiza NEMC
kukifunga kiwanda hicho mpaka mapendekezo yaliyotolewa na Baraza
yatakapokamilika. "Kiwanda hiki kisitishe shughuli za uzalishaji mpaka
pale vigezo vya Sheria ya Mazingira vitakapokamili"
Katika hatua nyingine Waziri Makamba
ametembelea Ziwa Chala na kuwataka wadau wa mazingira kuongeza jitihada katika
kulihifadhi kwa kuwa ni muhimu kwa
ikolojia na historia yake. " Kina cha ziwa hili kinashuka kwa kasi
kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi na sisi kama Serikali
tutahakikisha tunawekeza nguvu zetu katika kunusuru kina cha ziwa hili
kisiendelee kushuka" Alisisitiza Makamba.
Waziri Makamba ameahidi kuzungumza
na Serikali ya Kenya ili kuwa na mikakati ya pamoja ya kuhifadhi ziwa hilo kwa
kukuwa lipo pande zote za nchi hizi. Ziwa Chala ni chanzo kikubwa cha utalii na
limetokana na mlipuko wa Volcano likiwa halitoi wala kuingiza maji kutoka
vyanzo mbalimbali.
Waziri Makamba amemaliza ziara yake
Mkoani Kilimanjaro na hii leo amewasili Mkoani Arusha.
No comments:
Post a Comment