Kocha
Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Mayanga leo
Jumatatu Machi 13, 2017 ametangaza majina ya wachezaji 26 watakaounda kikosi
hicho.
Taifa
Stars, inatarajiwa kucheza na Botswana Machi 25, 2017 kabla ya kuivaa Burundi
Machi 28, mwaka huu katika michezo kirafiki wakati huu wa Kalenda ya Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Katika
mkutano wake na wanahabari uliofanyika leo Makao Makuu ya TFF, yalioko Uwanja
wa Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, Mayanga aliwataja wachezaji hao kuwa ni
walinda milango, Aishi Manula (Azam
FC), Deogratius Munishi (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).
Walinzi
wa pembeni upande wa kulia aliwataja Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto
wapo Mohammed Hussein (Simba) na Gadiel Michael (Azam FC).
Mayanga
aliwataja walinzi wa kati Vicent Andrew (Yanga SC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar),
Abdi Banda (Simba SC) na Erasto Nyoni (Azam
FC) ilihali aliwataja viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude (Simba SC).
Kadhalika
wako viungo wa kushambulia Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC), Frank Domoyo (Azam FC) na Muzamil
Yassin (Simba) wakati viungo wa kulia waliotajwa ni Simon Msuva (Yanga SC) na Shizza Kichuya (Simba SC).
Viungo wa kushoto ni Farid
Mussa (Teneriffe, Hispania) na Hassan Kabunda (Mwadui
FC) wakati washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC
Genk- Ubelgiji), Thomas Ulimwengu na AFC
Eskilstuna – Sweden), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu(Kagera Sugar) na Abdul-Rahman
Mussa (Ruvu Shooting).
Pia
Mayanga aliwataja wasaidizi wake kuwa Kocha Wa Makipa, Patrick Mwangata wakati
Meneja wa timu upande wa ufundi atakuwa mwenyewe Mayanga na upande wa mipango
mingine atakuwa Danny Msangi; Mtunza Vifaa, Ally Ruvu wakati Daktari wa timuatakuwa
Richard Yomba huku Daktari wa viungo akiwa
ni Gilbert Kigadya.
Timu
hiyo itaingia kambini Machi 19, 2017 kwenye Hoteli ya Urban Rose, Dar es Salaam
na mara baada ya michezo hiyo kambi itaahirishwa Machi 29, mwaka huu.

No comments:
Post a Comment