Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,
Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (katikati) akiweka
saini katika kitabu cha wageni alipofanya ziara Kituo cha Afya cha
Kabyaile-Ishozi kuona hali halisi ya ujenzi wa majengo mapya ya kituo hicho
mara baada ya athari za Tetemeko la Ardhi Kagera, wa kwanza kulia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt.Hamisi Mwinyimvua na kulia kwake ni. Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe.
Maj.Gen.(Mstaafu)Salum Kijuu.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Maj.Gen.(Mstaafu)Salum Kijuu akitoa neno la ufunguzi wa kikao wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama mkoani Kagera iliyofanyika Tarehe 17 Machi, 2017.
Baadhi ya Wajumbe wa kikao cha kupokea Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi iliyoathiriwa na Tetemeko la Ardhi Kagera wakifuatilia taarifa iliyowasilishwa na Kamishna wa Polisi Bw.Diwani Athuman (hayupo pichani) wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama Machi 17, 2017
Kamishna wa Polisi Bw.Diwani Athuman akiwasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Miradi yote inayoendelea kushughulikiwa ikiwa ni sehemu ya kurejesha hali mara baada ya kutokea kwa Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera wakati wa Ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama Machi 17, 2017
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb)akisalimiana na baadhi ya watumishi wanaoshughulika na ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kabyaile-Ishozi baada ya Athari za Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera.
Muonekano wa baadhi ya majengo ya Kituo cha Afya cha
Kabyaile-Ishozi kilichojengwa mara baada ya kituo kilichokuwepo kuathiriwa na
Tetemeko la Ardhi mkoani Kagera.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akitoa maagizo kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Maj.Gen.(Mstaafu)Salum Kijuu wakati wa ziara yake mkoani Kagera kukagua ujenzi wa majengo yaliyoathiriwa na Tetemeko la Ardhi.
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uratibu) Dkt.Hamisi Mwinyimvua (katikati)
akiangalia ubora wa madirisha yaliyowekwa katika Kituo cha Kulea Wazee cha
Kiilima mara baada ya ukarabati kutokana na athari za Tetemeko la Ardhi mkoani
Kagera
Mkazi wa Kituo cha Kulelea Wazee cha
Kiilima Bw. Frednand akimweleza Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama manufaa
ya kuboreshwa kwa kituo hicho mara baada ya kuathiriwa na Tetemeko la Ardhi
wakati wa ziara yake kituoni hapo Machi
17, 2017.
Kaimu Mkuu wa Kituo Kulelea Wazee cha Kiilima Bi. Gaudencia
Rwiza akipokea magunia ya mchele na mafuta ya kupikia yaliyotolewa na Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe.
Jenista Mhagama wakati wa ziara yake kituoni hapo. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mhe. Maj.Gen.(Mstaafu)Salum Kijuu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akikagua vifaa vilivyohifadhiwa stoo ya Shule ya Sekondari ya Nyakato wakati wa ziara yake shuleni hapo ili kuona maendeleo ya ukarabati wa shule hiyo mara baada ya shule kuathiriwa na tetemeko la ardhi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na
Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa
Shule ya Omumwani inayo wajumuisha wanafunzi kutoka Nyakato na Ihungo Sekondari
mara baada ya Athari za Tetemeko la Ardhi lililotokea mkoani Kagera wakati wa
ziara yake Machi 17, 2017.
PICHA
ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU












No comments:
Post a Comment