Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison George Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari Mjini Dodoma (hawapo Pichani) kuhusu agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kuachiwa huru kwa msanii wa Muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki (Ney wa Mitego) Kulia ni Naibu Waziri wake Mhe. Anastazia Wambura.
***********************************
*Amshauri aboreshe wimbo wake zaidi.
*Amesema ni haki yake ya kujieleza.
Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameliagiza Jeshi la Polisi kumwachia huru msanii wa muziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki maarufu kama Ney wa Mitego kutokana na wimbo wake Wapo unaosadikiwa kukiuka madili.
Akitoa kauli hiyo kwa niaba ya Rais Magufuli, Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison George Mwakyembe amesema kuwa Msanii huyo ametumia haki yake ya kikatiba ya kujieleza na ni Haki ya kila Mtanzania kujieleza kwa namna moja au nyingine pasipo kuvunja katiba ya Nchi.
Waziri Mwakyembe amesema Mwanamuziki huyo ni Mmoja kati ya wanamuzi wanaopendwa sana na Mhe Rais kutokana na kazi zake za muziki zinazoelimisha na kueleza changamoto mbalimbali zinakumba taifa letu.
“Mhe. Rais anaupenda wimbo wa msanii huyu na ameshauri auboreshe zaidi asipunguze chochote ila aongezee tu tabia nyingine ambazo hajazitaja katika wimbo wake” alisisitiza Dkt Mwakyembe.
Aidha Mhe. Waziri ameeleza kuwa Mhe Rais ametoa ushauri kwa msanii huyo kuboreshe wimbo huo zaidi kwani mengi aliyoyaongelea katika wimbo wake yanatokea katika jamii na kutolea mfano kama akiboresha na kuelezea zaidi kuhusu wakwepa kodi,wauzaji, wasambazaji na watumiaji madawa ya kulevya,na watanzania wasipoenda kufanya kazi kwani makundi haya yote yapo katika jamii.
MAFOTO PRODUCTION & ENTERTAINMENT KWA MAHITAJI YAKO YA STILL PICTURE, VIDEO SHOOTING, MUSIC & Mc's KATIKA SHEREHE YA AINA YEYOTE. VIDEO EDDITING, COVER DISGNING, PPS ZA DK 3, POSTERS ZA AINA MBALIMBALI COVER CD PRINTING, BURNING CD N.K. WASILIANA NASI KWA NO, 0787 200005/0754, 0655-306109/0714 656660 BARUA PEPE:- muhidinuk@yahoo.co.uk,sufianimafotoblog@gmail.com AMA TEMBELEA www.sufianimafoto.com
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania March 3, 2025,nakukaribisha
kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini
ke...
-
[image: Tumore prostatico: la prognosi in base a stadio, grado e rischio]
Tumore prostatico: la prognosi in base a stadio, grado e rischio
alt=”” class=”w...
DIAMOND PLATINUMZ HOUSE 'STATE HOUSE'
-
Bila shaka muziki unalipa na ndio maana mwanamuziki wa Bongo Fleva, kutoka
Tanzania Naseeb Abdul 'Diamond Platnumz, ameweza kujenga nyumba jambo
ambal...
No comments:
Post a Comment