MABAO mawili ya kila kipindi yaliyofungwa na
washambuliaji, Simon Msuva na Mbaraka Abeid yalitosha kuipa ushindi wa mabao 2-1 Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ dhidi ya Burundi,
katika mchezo wa Kimataifa wa Kirafiki uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini
Dar es Salaam,jioni ya leo.
Ushindi huo ni wa pili ndani ya siku tatu baada ya
Jumamosi iliyopita kuifungaa timu ya Taifa ya Botswana kwa bao 2-0.

Katika mchezo wa leo, Stars ilimkosa nahodha wake, Mbwana
Samatta ambaaye alicheza kwenye mchezo wa Jumamosi na kuiwezesha Stars kuibuka
na ushindi huo wa mabao mawili ambayo
yote yalifungwa Samatta.
Stars ilipata bao lake la kwanza katika dakika ya 20 ya
kipindi cha kwanza kupitia kwa Msuva aliyetumia vizuri pasi safi ya kichwa
kutoka kwa Ibrahim Ajib.
Stars ambayo haikuwa kwenye ubora wake ukilinganisha na
mchezo uliopita, iliwapumzisha baadhi ya wachezaji wake waliocheza mchezo uliopita.

Stars ilienda mapumziko ikiwa mbele kwa bao 1-0 lakini
iliwachukua Burundi dakika nane tu tangu kuanza kwa kipindi cha pili
kusawazisha bao hilo kupitia kwa Laudit Mavugo aliyetumia vizuri makosa ya beki
wa kati wa Stars, Abdi Banda.
Kinda aliyetokea benchi, Mbaraka Abeid, kipindi cha pili
kuchukua nafasi ya Farid Mussa, aliwainua tena mashabiki wa Stars kwa kutupia bao
la pili baada ya kuuwahi mpira uliopigwa kutoka nyuma na kumchambua kipa wa
Burundi na mpira kugonga mwamba kabla haujamrudia tena Mbaraka na kuukwamisha
wavuni.
Matokeo ya Mchezo huo wa Kimataifa wa kirafiki, huenda yakaipandisha
Tanzania kwenye viwango vya ubora vinavyotolewa
na Shirikisho la soka Duniani (FIFA). KWA MATUKIO ZAIDI YA PICHA ZA MTANANGE HUU KAA NASI HAPO BAADAYE.

No comments:
Post a Comment