Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, wazee na watoto imebainisha kuwa inatarajia
kuwapeleka Madaktari wake waliopo nchini Tanzania kwenda kufanya kazi nchini
Kenya kufuatia kuombwa na Rais wa nchi hiyo Mhe. Uhuru Kenyatta.
Akizungumza na vyombo vya habari mapema
leo, Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu amesema kuwa, ujumbe maalum kutoka kwa
Rais Uhuru Kenyatta kupitia kwa Wiziri wake wa Afya uliokutana na Rais wa
Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli na
kuomba ombi lao hilo la kutaka madaktari 500, ambao wataajiliwa kwa mikataba
maalum ya kuanzia miaka 2 kwa kufanya kazi nchini Kenya.
“Natoa rai kwa madaktari wazawa waliopo
nchini kuomba nafasi za ajira ya Udaktari
nchini Kenya kwa mkataba maalum. Zoezi hilo limeanza rasmi leo Machi 18
mpaka Machi 27, mwaka huu wawe wameomba.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa waombaji ni
wale watakaokidhi vigezo maalum ikiwemo asiwe katika utumishi wa Umma, Asiwe
amejiliwa na mashirika ya umma ama mashirika teule ambayo yanalipiwa na
Serikali.
Kwa Mujibu wa Waziri Ummy ameeleza kuwa
muombaji lazima awe amehitimu mafunzo ya “internalship” na mwisho awe
amesajiliwa na baraza la Madaktari
nchini.
Aidha, Waziri Ummy ameweka wazi kuwa, ajira
hiyo itakuwa ni ya miaka miwili ambapo watapata mishahara na malupulupu
mbalimbali katika ajira zao hizo huku akibainisha kuwa, jambo hilo ni jema na
linaiingizia Taifa sifa kwa kupeleka wataalamu wake nje ya nchi kupata ajira.
Kwa upande Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
Dk. Mpoki Ulisubisya amesema kuwa, moja ya vigezo ambavyo vinahitajika kwa
madaktari hao ni pamoja na kuwa na digrii ya kwanza na Internal ship huku
akiongeza kuwa, kwa upande wao Wizara imejipanga kuimalisha madaktari wa ndani
ikiwemo kiwaajili.
Naye Katibu Mkuu Utumishi, Mh. Laulian
Ndumbalo amewatoa hofu watanzania licha ya kuwapeleka Madaktari hao nje
kupatiwa ajira, nchini bado ina Madaktari wengi wanaofikia zaidi ya 1000, huku
kila mwaka wakiajili Madaktari 400 hadi 450.
Imeelezwa kuwa Madaktari hao watakaojitokeza watapata faida
kubwa kwani watakuza mahusiano mema ya nchi za Afrika Mashariki kupitia kada
hiyo huku pia wakitarajia kuipatia maendeleo nchi ya Tanzania. Jambo ili ndio
la kwanza linafanyika huku ikielezwa kuwa idadi hiyo ya madaktari kutoka
Tanzania kwenda kupatiwa ajira nje ya mipaka yake ni kubwa, licha ya madaktari
wengi kuwepo nchi mbalimbali ikiwemo Malawi, Zambia, Afrika Kusini, Botswana na
mataifa mengine.
Madaktari hao wenye kutaka kujiunga
wanaweza kutembelea tovuti ya wizara ya Afya na kupata maelezo mbalimbali.
No comments:
Post a Comment