Baadhi ya nyumba
zilizopo Mpigi darajani ambazo zinatakiwa kubomolewa kutokana na kujengwa ndani
ya mita sitini kutoka katika chanzo cha maji. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu
wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) amegiza wenye
nyumba hizo wabomoe kwa gharama zao wenye.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.)
akiongea na wananchi wa eneo la Mpigi darajani (hawapo pichani) na kusisitiza
katazo la kufanya shughuli zozote za kibinadamu ndani ya mita sitini. Kushoto
ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Bi. Fatuma Latu
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.) alipotembelea Mamlaka ya Usafi na Mazingira Chalinze kujionea changamoto za uchafuzi wa mazingira katika mto Wami.
***********************************************************
Na Lulu Mussa, Bagamoyo - Pwani
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba
ameagiza kusitishwa mara moja kwa shughuli zote za kibinadamu kando kando ya
Vyanzo vya maji.
Rai
hii imetolewa leo na Waziri Makamba mara baada ya kufanya ziara ya kukagua hali
ya mazingira katika Mkoa wa Pwani eneo la Mto Mpiji ambao umeathirika kutokana
na Uchimbaji wa mchanga na mmomonyoko wa ardhi unaohatarisha maisha ya wakazi
wa eneo hilo.
Waziri
Makamba amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo Bi. Fatuma Latu
kuwaondoa watu wote waliojenga pembezoni mwa Mto Mpiji na kuhakikisha zoezi
hilo linafanyika ndani ya siku 30. " Mkurugenzi hakikisheni kuwa wakazi
hao waliovamia eneo la mto huu na kujenga makazi yao ya kudumu wanaondolewa mara
moja" Alisisitiza Waziri Makamba.
Katika
hatua nyingine Waziri Makamba ametembelea Mto Wami na kusikitishwa na uharibifu
mkubwa wa mazingira unaosababishwa na shughuli za kibinadamu ikiwa ni pamoja na
kilimo, ufugaji na uchimbaji haramu wa madini, upasuaji mbao na uchomaji mkaa
unaopelekea mmomonyoko wa udongo na mchafuko/tope jingi na kusababisha kupungua
kwa uzalishaji wa maji.
Katika
kukabiliana na changamoto zilizoainishwa Waziri Makamba amesema Ofisi yake
itaanda kikao kazi kitakachojumuisha wadau wote muhimu ili kunusuru Mto Wami
haraka iwezekanavyo. "Serikali haiwezi kuwekaza fedha nyingi kwenye mradi
mkubwa kama huu na kuona uharibifu ukiendelea na kuharibu miundombinu, hali hii
haikubaliki na nitachukua hatua za haraka.
Waziri wa Nchi,
Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. January Makamba (Mb.)
yuko katika ziara ya kikazi katika mikoa Pwani, Tanga, Kilimanjaro, Arusha,
Manyara na Singida kujionea hali ya mazingira na changamoto za hifadhi katika
mikoa husika. Hii ni ziara ya pili baada ya iliyofanyika mwezi Oktoba 2016,
katika mikoa ya Nyanda za juu Kusini. Katika siku ya kwanza
Waziri Makamba ametembelea Mto Mpigi, Mto wami na hifadhi ya msitu wa Kibindu
uliovamiwa na wananchi.
No comments:
Post a Comment