Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh.Profesa Makame Mbarawa akikagua mojawapo
ya injini ya kivuko cha MV KAZI wakati wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya
ujenzi wa kivuko hicho. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kampuni ya MS Songoro
Marine Boatyard na Mtendaji Mkuu wa TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu. Kivuko hiki
kitakapokamilika kitatoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni.
Muonekano
wa kivuko kipya cha MV KAZI kinachotengenezwa na Kampuni ya MS Songoro Marine
Boatyard kikiwa katika hatua za mwisho kukamilika wakati wa ziara ya Mh.Profesa
Makame Mbarawa katika eneo la ujenzi wa kivuko hicho bandarini Dar es Salaam.
Kivuko hiki kitakapokamilika kitatoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni.
Mkurugenzi
wa kampuni ya MS Songoro Marine Boatyard Major Songoro akimuonyesha Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Mh.Profesa Makame Mbarawa alama za kuendeshea kivuko kipya
cha MV KAZI kitakachotoa huduma kati ya Magogoni na Kigamboni. Nyuma yake
ni Dkt. Mussa Mgwatu Mtendaji Mkuu wa Wakala
wa Ufundi na Umeme TEMESA.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mh.Profesa Makame Mbarawa akiwasili katika
kivuko cha MV KAZI kukagua maendeleo ya ujenzi wa kivuko hicho, kushoto kwake
ni Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu na nyuma
yao ni Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko TEMESA Mhandisi
Japhet Maselle. Kivuko hiki kitakapokamilika kitatoa huduma kati ya Magogoni na
Kigamboni. Picha na ALFRED S
MGWENO – TEMESA

No comments:
Post a Comment