Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiongeza wakati wa ufunguzi wa Jukwaa la Fursa za Kibiashsra lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa hilo lilijadili fursa mbalimbali za kibiashara zinazopatikana Mkoani Tanga.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Martin Shigela akitoa neon la
utangulizi wakati wa ufunguzi wa ufunguzi wa Jukwaa la Fursa za Kibiashsra
lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa hilo lilijadili fursa mbalimbali za
kibiashara zinazopatikana Mkoani Tanga
Mhariri Mtendaji wa Tanzania Standard Newspapers Dkt.
Jim Yonaz akielezea kuhusu malengo ya kongamano la Jukwaa la Fursa za
Kibiashsra lililofanyika leo Jijini Tanga. Jukwaa hilo lilijadili fursa
mbalimbali za kibiashara zinazopatikana Mkoani Tanga.
******************************************
Na
Mwandishi Wetu-MAELEZO
Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezi, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe amewataka wakazi wa
na wafanyabiashara wa Mkoa wa Tanga kuanza mapema kuzitumia fursa zilizopo
katika mkoa huo kabla ya wageni hawajazitu,ia na kuwaacha wenyeji kuwa
watazamaji.
Waziri Mwakyembe ametoa
rai hiyo leo Jijini Tanga wakati akifungua kongamano la siku moja la Fursa za
Biashara ambalo lina lengo la kufungua fursa za biashara zilizopo katika mkoa
na hasa katika kipindi hiki ambacho ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima
nchini Uganda hadi Chongoleani jijini Tanga unatarajiwa kuanza.
“Tusipojipanga leo na
kuzitumia vizuri hizi fursa nyingi zilizopo basi tujue fursa hizi zitatumiwa na
wageni ili hali Watanzania tunaauwezo”, alisisitiza Waziri Mwakyembe.
Alieleza kuwa kama kuna
changamoto zozote zinazowakabili watu wa Tanga na Watanzania kwa ujumla katika
kutumia fursa zilizopo basi ni vema Serikali ya Mkoa, wafanyabishara na
wawekezaji waliopo mkoa wa Tanga wakazitafutia ufumbuzi changamoto hizo ili
zigeuke kuwa fursa ili Watanzania wazichangamikie.
Aidha Mwakyembe
amewasisitiza Watanzania kuwekeza katika biashara ya huduma na viwanda vya
uzalishaji bidhaana bidha ambapo vitakuwa vikihudumia ujenzi wa miradi
mbalimbali hususani bomba la mafuta kutoka Hoima-Uganda hadi Chongoleani-Tanga,
Tanzania.
Ameeleza kuwa hivi sasa
kasi ya wageni kutaka kutumia fursa za bomba la mafuta imekuwa kubwa ambapo
ameeleza kuwa kuna baadahi ya wafanyabiashara kutoka nchi jirani wamekuwa
wakifanya ushawishi ili wafanyakazi na wataalamu watakaokuwa katika mradi wa
bomba la mafuta wawe wanatumia huduma za hoteli za nchi hiyo.
Akiongea awali, Mkuu wa
Mkoa wa Tanga, Martin Shigela alieleza kuwa wananchi wa Mkoa wa Tanga
wameendelea kujipanga kuhakikisha wanazitumia vizuri fursa zilizopo Tanga kwa
ajili ya kukukuza kipato na uchumi wa mkoa wa Tanga.
“Tumejiandaa vya kutosha
na wakati ni sasa na hatuna sabababu za kuchelewa kutumia fursa zilizopo”,
alieleza Mkuu wa Mkoa huku akitaja baadhi ya uwekezaji unaotarajiwa kufanywa ni
pamoja na ujenzi wa kiwanda kipya cha Saruji, ujenzi wa hoteli, kilimo, upanuzi
wa uwanja wa ndege na uimarishaji wa miundombinu ya reli na bandari.
Kwa upande wake, Mhariri
Mtendaji wa Tanzania Standard Newspapers (TSN), Dkt. Jim Yonaz aliwataka
wananchi na wafanyabiashara wa mkoa wa Tanga kuhakikisha kuwa wanakuwa na haki
na wajibu wa kushiriki kikamilifu katika kutumia fursa za ukuaji wa uchumi wa
mkoa ili wawe sehemu ya fahari ya kuirudisha Tanga ya viwanda kama ilivyokuwa
miaka ya nyuma.
Dkt. Yonaz alieleza kuwa
kuwa TSN wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inashirikiana na Serikali ya mkoa
kwa kutoa elimu kupitia magazeti ya Daily News na HabariLeo kutangaza fursa
mbalimbali zilizopo mchini ili wananchi waweze kuzifahamu na kuzifanyia kazi.
Jukwaa la Fursa za
Kibiashara linaloandaliwa TSN ni la kwanza kufanyika katika mkoa wa Tanga na la
tatu kufanyika hapa nchini ambapo la Jukwaa la kwanza lilifanyika mkani Simiyu
na lile la pili lilifanya mkoa wa Mwanza. Aidha kwa mujibu wa waandaji, jukwaa
kama hili linatarajiwa kufanyika hivi karibuni Visiwani Zanzibar na baadae
katika mkoa wa Arusha.
No comments:
Post a Comment