WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo kuhusu Mkakati wa Viwanda na mpango kazi wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Africa (SADC) baada kumalizika kwa mkutano wa 37 wa SADC uliomalizika hivi karibuni nchini Afrika ya Kusini. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Msaidizi, Idara ya Mtangamano wa Biashara, Sekela Mwaisela na Kaimu Mkurgenzi Idara ya Uwekezaji, Aristides Mbwasi.
MKAKATI WA VIWANDA NA MPANGO KAZI WA JUMUIYA YA MAENDELEO
KUSINI MWA AFRIKA-SADC (INDUSTRIALIZATION STRATEGY AND ROADMAP AND ACTION PLAN
FOR SADC, 2015-2063)
Mkakati wa Viwanda wa
SADC kwa mwaka 2015-2063 ulipitishwa mjini Harare, Zimbawe tarehe 29 Aprili,
2015, katika mkutano wa dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC. Mkakati
huu unalenga kuzifanya nchi za SADC kuwa na uchumi wa viwanda na kushiriki
zaidi katika mnyororo wa thamani kikanda na kimataifa (Regional and Global
Value Chains) na hivyo kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi wake.
1.1 Nguzo za Mkakati wa Viwanda
Mkakati wa kuendeleza Viwanda
katika Nchi za SADC una nguzo tatu
(3) zinazotegemeana ambazo ni:
(i)
Uendelezaji
viwanda kama njia ya kuleta mageuzi ya kiuchumi (Industrialization as a champion
of economic transformation);
(ii)
Kukuza
ushindani (enhancing competitiveness); na
(iii)
Kuongeza
utangamano wa kikanda.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
1.2 Maeneo Makuu Yaliyoainishwa kwenye Mkakati
Mkakati umeainisha
maeneo makuu (Clusters) sita (6) ambayo Nchi za SADC zinaweza kuyatumia katika
kukuza ushiriki wao kwenye mnyororo wa thamani na hivyo kuongeza ushiriki wa
nchi hizo kwenye masoko ya kikanda na kimataifa. Maeneo hayo ni kama ifuatavyo:
(i)
Usindikaji
mazao ya Kilimo (Agro-processing);
(ii)
Shughuli
zinazoendana na Uchenjuaji Madini (Minerals and mineral benefication)
(iii)
Madawa
ya Binadamu (Pharmaceuticals);
(iv)
Uzalishji
Bidhaa zinazotumiwa mara kwa mara (Manufacturing of Consumer Goods);
(v)
Bidhaa
za Uwekezaji (Capital Goods); na
(vi)
Huduma
(Services).
2. MPANGO KAZI WA KUENDELEZA VIWANDA KATIKA NCHI ZA SADC
Mpango Kazi wa
kutekeleza Mkakati wa kuendeleza Viwanda (Action
Plan for implementation of SADC Industrialization Strategy and Roadmap) ulipitishwa
katika mkutano usiokuwa wa kawaida wa Wakuu wa nchi na Serikali uliofanyika
mwezi Machi, 2017 huko Lozitha Swaziland. Mpango kazi huo utatekelezwa katika
kipindi cha miaka kumi na tano (15) kuanzia mwaka 2015 - 2030 kama awamu ya
kwanza.
Mpango kazi huo
umegawanyika katika maeneo makuu matano (5) ambayo yanajumuisha maeneo matatu
ya kimkakati. maeneo mengine yaliyoongezwa ili kurahisisha utekelezaji wa Mkakati
huo kama yafuatavyo:
(i)
Uendelezaji
viwanda kama njia ya kuleta mageuzi ya kiuchumi (Industrialization as Champion
of Economic Transformation);
(ii)
Kukuza
ushindani (enhancing competitiveness);
(iii)
Kuongeza
utangamano wa kikanda (Regional Integration);
(iv)
Masuala
Mtambuka (Crosscutting issues); and
(v)
Tathmini
na Ufuatialiaji (Monitoring and Evaluation).
Nchi
wanachama wanawajibika moja kwa moja kwenye vipengele vinavyohusu masuala ya
ndani ya nchi hususan Uandaaji wa Sera Wezeshi, Utafiti; Kuunganisha sekta ya
viwanda na sekta nyingine na kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji kwenye
viwanda. Sekretariati ya SADC imekuwa na majadiliano na wahisani mbalimbali kwa
ajili ya kuwaomba kuwezesha utekelezaji wa Mkakati huu. Baadhi ya Wahisani
wamethibitisha kufadhili utekelezaji wa baadhi ya maeneo ya mkakati kama yafuatavyo:
(i)
Kuongeza
Thamani Mazao ya Kilimo na Kuwajengea Uwezo Wajasiriamali;
(ii)
Uchenjuaji
Madini na Kuongeza Thamani Madawa ya Binadamu
(Pharmaceuticals); na
(iii)
kujengea
uwezo Wajasiriamali kuhusu Mpango wa Kueneza Mkakati wa kuendeleza viwanda katika
Nchi za SADC.
MAENEO
AMBAYO YAMEAINISHWA NCHINI TANZANIA KUWA NA FURSA KATIKA KUTEKELEZA MKAKATI
VIWANDA KATIKA NCHI ZA SADC
Tathamini
ya ushiriki wa nchi moja moja kwenye maeneo sita yenye fursa za kuongeza
thamani (clusters) yaliyoanishwa hapo awali ilizingatia shughuli za kuongeza
thamani zinazoendelea ndani ya nchi husika hivi sasa na uwezekano wa kuibua
shughuli nyingine kutokana na rasilimali, sera na mazingira ya uzalishaji
yaliyopo ndani ya nchi husika kwa kulinganisha na nchi nyingine za SADC.
Kufuatia
vigezo hivyo, Tanzania imeainishwa kuwa na ushindani mzuri katika maeneo matano
(5) kati ya sita (6) yaliyoanishwa kama yafuatavyo:
Jedwali
1: Maeneo ambayo Tanzania imeainishwa kuwa na fursa katika kutekeleza Mkakati
wa kuendeleza Viwanda katika Nchi za SADC
|
NA
|
ENEO (CLUSTER)
|
FURSA ZA VIWANDA
ZILIZOPO NA ZINAZOWEZA KUANZISHWA
|
|
1.
|
Usindikaji
Mazao ya Kilimo
|
Sukari,
mihogo, bidhaa za maziwa, bidhaa za nafaka, bidhaa zinazotokana na mbegu za
mafuta na bidhaa zainazotokana na misitu
|
|
2.
|
Shughuli
zinazoendana na uchenjuaji madini
|
Madini
ya Chuma; base-metals (shaba, aluminium, nikeli na Kobalti);
mbolea; saruji; magadi;
|
|
3.
|
Madawa
ya binadamu
|
ARV;
Dawa za Malaria; Vyandarua
|
|
4.
|
Uzalishaji
bidhaa zinazotumiwa mara kwa mara
|
Bidhaa
za ngozi; viatu
|
|
5.
|
Utoaji
huduma
|
Utalii
|
|
6.
|
Bidhaa
za uwekezaji: Mashine na vifaa
|
Hakuna
|
Manufaa
kwa Tanzania yanayotokana na Mkakati huu
Tanzania itanufaika
kwa kutekeleza miradi mbalimbali na hivyo kuongeza kasi ya kufikia malengo ya
nchi kama ifuatavyo.
- kushiriki
katika mnyororo wa thamani kikanda
na kimataifa (Regional and Global Value Chains) na hivyo kuongeza kasi ya
maendeleo kwa wananchi wake na kuafanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa
viwanda; na
- Mkakati huu
utaisaidia Tanzania kushiriki na kunufaika zaidi na wigo mkubwa wa masoko
ya kikanda na kimataifa.
- Tanzania
itanufaika na Transfer of Technology
kutoka nchi wanachama wa SADC.
- Kwa kupata ufadhili Tanzania itatumia malighafi
yanayopatikana humu nchini kuzalisha bidhaa zitakazoshindana katika Kanda
na kukuza ushindani.
3. MAENEO AMBAYO MKAKATI WA SADC UNAWIANA NA MKAKATI WA
KUHARAKIWA UENDELEZAJI WA VIWANDA NCHINI
Mkakati
wa Viwanda wa SADC unakuja katika muda muafaka kwa Tanzania, kwa vile unaendana
na Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa
nchi unayolenga Tanzania kuwa na uchumi wa Viwanda. Aidha, Mkakati huo
unaendana na Mkakati wa kuharakisha
uendeleza viwanda ulioandaliwa na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji,
kwenye maeneo makuu yafuatayo:
|
Na.
|
Mkakati wa Viwanda
wa SADC
|
Mpango wa Pili wa Miaka Mitano
|
|
(i)
|
Kuongeza
ajira hadi asilimia 40 kufikia mwaka 2030
|
Ukuaji
ajira utakuwa kufikia asilimia 5.4 ifikapo mwaka 2020; na katika Malengo
ya ilani ya chama cha mapinduzi ya
2015 malengo ya sekta ya Viwanda ni
kuchangia asilimia 40 ya ajira zote kufikia mwaka 2020
|
|
(ii)
|
Bidhaa
zinazotumiwa mara kwa mara (Manufacturing: consumer goods) wa SADC utakua kwa
asilimia 30 ifikapo 2030
|
Kasi ya ukuaji wa Sekta ya Viwanda utaongezeka kwa wastani wa asilimia 10.5
ifikapo mwaka 2020
|
|
(iii)
|
Unatoa kipaumbele katika Mnyororo
wa Thamani na uongezaji thamani mazao ya Kilimo na yasiyokuwa ya Kilimo
|
Kuongeza thamani mazao yote yanayosafirishwa
nje ya nchi
|
|
(iv)
|
Unatekelezwa kwa kushirikisha sekta
nyngine kama vile Kilimo, Madini, Uchukuzi, miundombinu, Rasilimali watu n.k.
na Sekta Binafsi imeshirikishwa kwa
kuwa ndio wanaotekeleza Mkakati huo
|
Unatekelezwa kwa kushirikisha sekta
nyingine
|
TANZANIA ILIVYOJIPANGA KUTEKELEZA MKAKATI
WA VIWANDA.
MIRADI AMBAYO
IMESHAPATA UFADHILI NA AMBAYO INATEGEMEA KUPATA UFADHILI KWENYE MKAKATI WA VIWANDA
i.
Katika kutekeleza Mkakati wa Viwanda, Tanzania kupitia
Sekretarieti ya SADC iliwasilisha miradi mbalimbali kuomba ufadhili, hivyo tumepata
ufadhili wa kiasi cha Euro 1,400 kutoka mfuko wa Jumuiya ya Ulaya ( European Development Fund-
EDF11). Ufadhili huo utasaidia kwenye miradi mine ikiwepo mradi wa kupitia upya Sera ya
Viwanda( Review of Sustainable Industrial Policy-1996-2020), na kuwezesha
mnyororo wa thamani wa Alizeti hususan kuimarisha masuala ya viwango na ubora(Upgrading
the Tanzania Sunflowers value chain; focusing on strengthening capacity on SPS and standards and quality Management
System. Maandalizi ya awali yameanza kama vile kuandaa activities zitazofanyika katika kipindi cha miezi miwili ijayo.
ii.
Mnyororo wa thamani
na kuongeza thamani kwenye mazao ya kilimo na mazao yasiyokua ya
kilimo(Value chain ana value addition on
Agriculture products and non non agriculture products)
SADC
Sekretarieti imeendelea kuhamasisha wafadhili mbalimbali kufadhili miradi ya kipaumbele. Sekretarieti inaendelea kujadiliana na International Cooperation Partners kusaidia miradi ya kipaumbele
iliyoainishwa katika mnyororo wa thamani
na uongezaji thamani ya mazao ya kilimo na yasiyokua ya kilimo. Tanzania
tuliwasilisha miradi ya sekta ya ngozi
na mazao yake, mbao na mazao yake na
sekta ya mavazi. Hata hivyo Secretarieti ya SADC inafanya utafiti kuainisha Sekta ya kipaumbele kwa Kanda nzima
na ripoti ya utafiti huo utakamilika
Desemba 2017.
iii) Mnyororo wa thamani kwenye sekta ya madini
na Madawa (Mineral and Pharmaceutical Value Chains)
SADC
Sekretarieti inatafuta ufadhili katika kuchenjua na kuongeza thamani Madini badala
ya kusafirisha madini hayo nje ya nchi
yakiwa ghafi. Mpaka sasa zoezi la kupata wafadhili unaendelea katika ngazi ya
Secretarieti ya SADC.
Kwa upande wa sekta
ndogo ya madawa, Tanzania iliwasilisha miradi ya kuwezeshwa katika kuzalisha wa
madawa ya magonjwa ya kuambukizwa na yasiyo ya kuambukizwa (Non communicable
and communicable diseases) ili waweze kuingia katika mnyororo wa thamani na
kuingia katika soko la Kikanda na Kimataifa. Sekretarieti ya SADC wanaendelea
kujadiliana na Wafadhili mbalimbali kuwezesha kutekeleza Mpango Kazi wa Viwanda
wa SADC
WIZARA YA VIWANDA,
BIASHARA NA UWEKEZAJI
AGOSTI 2017


No comments:
Post a Comment