RAIS wa Zimbabwe, Robert Mugabe, amejiuzulu nafasi yake ya urais rasmi.
Akitangaza taarifa hiyo Spika wa Bunge la Zimbabwe, amesema kuwa Rais Mugabe ameamua kutangaza kujiuzulu Urais wa nchi hiyo bila kuweka masharti yeyote.
Baada ya kutangazwa taarifa hiyo, Wananchi wa Zimbabwe, wameonekana mitaani wakishangilia, wakiimba na kucheza kufurahia hatua ya Rais wao Robert Mugabe aliyeongoza nchi hiyo tangu mwaka 1980.
***********************************************
IMEELEZWA kuwa mmoja ya watu wanaotarajiwa kumrithi rais Mugabe wa Zimbabwe amekimbizwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu kulingana na chombo cha habari cha AFP. Emmerson Mnangangwa ambaye ni makamu wa rais wa Zimbambwe alikuwa mgonjwa ghafla wakati wa mkutano wa hadhara siku ya Jumapili. AFP imemnukuu waziri wa Afya David Parirenyatwa akisema: Anaendelea kupata nafuu.
''Alikuwa akitapika na kuharisha na kukosa maji mwilini. Amefanya vipimo vingi''. Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 93 amesema kuwa atatetea wadhfa wake wakati wa uchaguzi wa mwaka ujao.
No comments:
Post a Comment