Habari za Punde

DKT. MWAKYEMBE AFANYA ZIARA ARUSHA ATOA NENO LIGI YA WANAWAKE

HAFLA ya uzinduzi wa Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake imezinduliwa jana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe kwenye Uwanja wa General Tyre jijini Arusha.
Timu zilizokata utepe zilikuwa ni Alliance Queens ya Mwanza iliyoshinda mabao 2-1 dhidi ya Panama FC ya Iringa.
Katika uzinduzi huo Waziri Dk. Mwakyembe aliwataka wachezaji wa timu zote kujituma kwa juhudi zaidi kwa kuwa mpira wa miguu kwa sasa ni ajira kubwa sana kwa vijana.
“Vijana wangu natambua mnapenda mpiwa wa miguu, naomba mzingatie vitu vitatu muhimu - nidhamu, juhudi na kujitunza,” amesema Waziri Dk. Mwakyembe akiwa na Rais wa TFF Wallace Karia, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Kidao Wilfred na viongozi wa FA Mkoa wa Arusha.
Mara baada ya kufanya uzinduzi huo, Waziri akiwa na viongozi hao leo ametembelea Uwanja wa Sheikh Amri Abeid kutazama maendeleo ya marekebisho yanayofanyika kwenye Uwanja huo.
Mbali na uwanja  huo pia waziri alifanya ziara fupi kwenye viwanja wmbalimbali ikiwa ni pamoja na kiwanja cha FFU kwa Morombo, Arusha  ambapo aliwapongeza kwa ukarabati mzuri wa nyasi za kuchezea.
Katika ziara nyingine Waziri pamoja na Viongozi wa TFF walitembelea shule ya Trust St. Patric Sports Academy ambacho ni kutuo cha kukuza michezo na timu zinazoshiriki ligi hiyo, zimeweka kambi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.