Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Dkt. Harrison Mwakyembe, (kulia), na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, wakiwaonyesha waandishi wa habari, tuzo ambayo PSPF ilinyakua katika mashindano ya kimataifa wakati wa mkutano wa taasisi ya hifadhi ya jamii Duniani, International social security association, taasisi tanzu ya ILO, tuzo ya ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017 mjini Adis Ababa Ethiopia mwezi uliopita. Tukio hili limefanyika pembezoni mwa mkutano wa kampeni ya uzalendo na utaifa iliyoongozwa na waziri Mwakyembe kwenye ukumbi wa mikutano wa PSPF jijini Dar es Salaam leo Novemba 25, 2017.
***********************************************************
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umenyakua tuzo ya kimataifa ya ISSA GOOD PRACTICE AWARDS AFRICA COMPETITION 2017, baada ya kuwa Mfuko unaotoa huduma bora kupitia ubunifu wa mafao ya muda mfupi, yaani service quality in short-term products.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuonyesha tuzo hiyo iliyokwenda sambamba na kampeni ya uzalendo na utaifa Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu alisema, Mfuko huo unajivunia kwa kuwa Mfuko wa kwanza miongoni mwa Mifuko mitano ya Hifadhi ya Jamii nchini, kuanzisha bidhaa na huduma za muda mfupi ambazo zimekuwa kivutio kikubwa kwa wanachama na hivyo kuvutia mifuko mingine ambayo kwa sasa nayo imeanza kutoa huduma hizo.
“Mwaka huu katika mkutano wake wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Duniani yaani International Social Security Association, taasisi tanzu ya Shirika la Kazi Duniani,(ILO) imeipatia PSPF tuzo baada ya kuwa Mfuko bora barani Afrika katika utoaji huduma bora kupitia ubunifu wa Mafao ya muda mfupi yaani service quality kwenye short-term products.” Alifafanua Bw. Mayingu.
Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe aliipongeza PSPF kwa kujinyakulia tuzo hiyo na kuliletea taifa heshima kubwa kimataifa.
“Kupambanishwa katika bara la Afrika na kushinda vigezo kadhaa ndipo unaambiwa bwana wewe unapata hii tuzo na tuzo hii imetolewa na taasisi yenye ushirikiano wa karibu sana na ILO hongereni sana.” Alipongeza Dkt. Mwakyembe.
Alisema ushirikiano wa karibu miongoni mwa wafanyakazi wa PSPF ndio umepelekea mafanikio hayo.
“Niwapongeze viongozi wote wa PSPF, Wafanyakazi wote wa PSPF, kwa kazi nzuri mnayoifanya mpaka mnatambuliwa na jumuiya ya Kimataifa.” Alisema.
Aidha kabla ya tukio hilo, Waziri aliwahamasisha watanzania kujenga moyo wa uzalendo na kujivunia utaifa wao kwani mambo hayo ni muhimu katika ujenzi wa taifa.
“Sisi tuliokuwepo kabla ya uhuru, niwaombe sana, tuwasaidie vijana wetu wa sasa kutambua tumetoka wapi, tuko wapi na tunaelekea wapi, kwa kujenga uzalendo wa kuipenda nchi yetu kama ambavyo ilikuwa hapo awali.” Alisema.
Kampeni hiyo inatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muunganmo wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli baadaye mwezi ujao mjini Dodoma, na Waziri aliwahamasisha wadau mbalimbali kujitokeza na kuchangia fedha ili kufanikisha swala hilo muhimu kwa taifa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyemba, akizungumza kuhusu umuhimu wa jamii kiujenga uzalendo wa taifa lao la Tanzania.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sanaa, Leah Kilimbi, akizungumzia maudhui ya hafla hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. ASdam Mayingu, akizunhgumza kwenye hafla hiyo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, akizungumza wakayti wa hafla hiyo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, ambaye pia ni Meneja Uhusiano wa Mfuko huo, Bi. Lulu Mengele, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Bw.Sami Khalfan, wakifuatilia hafla hiyo.
Meneja Uhusiano wa DAWASCO, Bi. Nelly Msuya akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mkurugenzi wa vipindi wa Azam TV, Bw. Charles Hillary, (kulia), akizungumza kwenye hafla hiyo.
Bw. Mayingu akizungumza huku akipongezwa kwa makofi na waziri Mwakyembe na Bi.Joyce Fisso, Katibu Mtendaji bodi ya Filamu Tanzania.
Afisa Uhusiano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, (NHIF), akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Bi. Grace Michael Kisinga.
Baadhi ya wageni waalikwa
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi. Joyce Fisso, akizungumza.
Baadhi ya wasanii waliohudhuria hafla hiyo
No comments:
Post a Comment