Bondia
Mtanzania Ibrahim Class (kushoto) akipambana na Koos Sibiya, kutoka Afrika
Kusini katika pambano la
kimataifa la ngumi la raundi 12 lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Katika pambano hilo Mtanzania Ibrahim Class, aliibuka mshindi kwa Pointi.
Waziri wa
Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) pamoja
na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo, Yusuph Singo (katikati)
na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa Bw. Mohamed Kiganja wakifurahia
pambano la ngumi kati ya mtanzania Ibrahim Class dhidi ya Koos Sibiya wa Afrika
Kusini lililofanyika jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akimpongeza Bondia Ibrahim Class baada ya kuibuka mshindi
katika pambano hilo. Kulia ni
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.Yusuph Singo.
Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.
Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari pamoja na
wananchi waliojitokeza katika pambano la ngumi la kimataifa kati ya mtanzania
Ibrahim Class pamoja na Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini lililofanyika jana
Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa
Bw. Mohamed Kiganja.
Mabondia wanawake
Felicha Mashauri (kushoto) akichapana na Happy Daudi wakati wa pambano la kimataifa kati ya Ibrahim Class wa hapa nchini dhidi ya
Koos Sibiya wa Afrika kusini.
Bondia Haidari Mchanjo akifurahia ushindi wa mizunguko sita alioupata dhidi ya Bondia Bakari Magona lililochezwa jana Jijini Dar es Salaam wakati wa pambano la kimataifa kati ya Ibrahim Class.
*********************************************************
Na Shamimu Nyaki-WHUSM.
Mwanamasumbwi Ibrahim
Class amewapa raha watanzania jana Jijini Dar es Salaam baada ya kumpiga Bondia
Koos Sibiya kutoka Afrika Kusini katika mtanange wa kimataifa baina yao uliokuwa
na mizunguko kumi na mbili.
Katika pambano hilo
lililohuzuriwa na Waziri wa Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe, Ibrahim Class alishinda katika
mzunguko wa kumi na mbili ambapo ameandika historia ya muda mrefu hapa nchini kwa mabondia
kutofanya vizuri katika mashindano ya Kimataifa.
Akizungumza baada ya
mchezo huo kumalizika Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo mhe. Dkt.
Harrison Mwakyembe amesema amefurahiswa sana na ushindi aliopata Ibrahim Class
na kuahidi kumpa ushirirkiano zaidi ili aendelee kufanya vizuri katika
mashindano mengine
“Siri ya mafanikio
katika Michezo ni kufanya mazoezi,kujiamini kusikiiza mafundisho ya mwalimu
pamoja na nidhamu,Ibrahim Class ni mwanamasumbwi anaepaswa kuigwa na mabondia
na wanamichezo wengine wote kutokana na uwezo wake wa kujituma hivyo
wanamichezo wanapaswa kuiga kutoka kwake ili wafanikiwe na kuitangaza nchi yetu
kimichezo.” Alisema Dkt. Mwakyembe.
Naye bondia Ibrahim
Class ameishukuru Serikali kwa ushirikiano iliyompa wakati wa mazoezi mpaka leo
amefanikiwa kupeperusha vyema Bendera ya Tanzania na ameahidi kuendelea kufanya
vizuri zaidi kila atakapokuwa ulingoni na kushinda mataji na mikanda mingi zaidi.
No comments:
Post a Comment