Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na
Michezo Bibi. Suzan Mlawi (wa kwanza kulia) akizungumza na wafanyakazi wa
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) leo Jijini Dar es Salaam ambapo
ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya kuandaa Kanzi Data ya wataalamu wa lugha ya Kiswahili.
Kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. Nicholous Willium.
Katibu Mkuu Bibi. Suzan Mlawi na Naibu Wake Bw.Nicholous Willium wa Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt.Seleman Sewangi (kulia) walipotembelea ofisi hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa
na Michezo Bibi. Suzan Mlawi akipokea Kamusi Kuu ya lugha ya Kiswahili kutoka
kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la
Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt.Seleman Sewangi katika
ofisi ya Baraza hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Bw.Nicholous Willium akipokea Kamusi Kuu ya lugha ya Kiswahili kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt.Seleman Sewangi katika ofisi ya Baraza hilo leo Jijini Dar es Salaam.
**************************************************************
Na: Shamimu Nyaki-WHUSM
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari,Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Suzan Mlawi amefurahishwa na hatua
iliyofikiwa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) la kuandaa Kanzi Data ya
Wataalamu wa Lugha ya Kiswahili ikiwa ni kutekeleza agizo la Mhe Waziri wa Wizara hiyo Dkt.Harrison Mwakyembe
alilolitoa kwa Baraza hilo hivi karibuni.
Bibi.Suzan ameyasema
hayo leo Jijini Dar es Salaam alipotembelea ofisi za Baraza hilo ambapo amesema
kuwa Kanzi Data hiyo itasaidia kuwatambua kwa urahisi watalamu wa lugha ya
Kiswahili waliopo hapa nchini ambapo watasaidia kukuza na kuendeleza lugha hii
kwa ufasaha ndani na nje ya nchi.
“Serikali ya awamu ya
tano ina jitihada kubwa sana kukuza na kuendeleza lugha yetu ya Kiswahili hivyo
sisi kama watendaji wa kufanikisha jitihada hizo ni wajibu wetu kuwatambua
wataalamu ambao wana uwezo wa kufanikisha adhma ya Serikali”.Alisema
Bibi.Suzan.
Kwa upande wake Katibu
Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt.Seleman Sewangi amesema
kuwa Baraza linaendelea kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili kwa ufasaha
kama moja ya majukumu yake ambapo linaendelea na utaratibu wa kuandaa mfumo
utakaotawatambua wataalamu wa lugha hiyo ambao wataisadia jamii kuelewa na
kutambua Kiswahili kwa ufasaha.
“Kama ilivyo jukumu la
Baraza la kukuza na kuendeleza lugha ya Kiswahili tumefanikiwa kuandaa Kamusi ya Kiswahili ambayo imeanza kutumika na
ina maneno ya Kiswahili fasaha ambayo watanzania wanapaswa kujifunza ili
wayatumie”.Alisema Dkt. Sewangi.
Kanzi Data ya Wataalamu
wa Kiswahili itasaidia wataalamu hao kujulikana ambapo watatakiwa kujisajili
kwa gharama nafuu lakini pia itasaidia Serikali kuwatambua na kuona jinsi
wanavyoweza kutumia elimu yao kukuza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi.
No comments:
Post a Comment