Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM) Livingstone Lusinde akiunguruma katika mkutano wa hadhara wa kumuombe kura mgombea Udiwani Kata ya Majengo wilayani Korogwe Mkoani Tanga Mustapha Shengwatu wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo zilizofanyika kwenye uwanja wa sabasaba wilayani Korogwe ambapo aliwataka wananchi kumchagua mgombea wa CCM.
Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM) Livingstone Lusinde kushoto akimnadi mgombea udiwani Kata ya Majengo Halmashauri ya Korogwe Mji kupitia Chama cha Mapinduizi (CCM) Mustapha Shengwatu kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Sabasaba sokoni wilayani humo.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga Allan Kingazi akizungumza katika uzinduzi huo wa kampeni kumuombea kura mgombea wa CCM Mustapha Shengwatu kupitia kata ya Majengo Halmashauri ya Korogwe Mji
Mwenyekiti wa CCM Korogwe Vijijini,Nassoro Hemedi Malingumu akizungumza katika mkutano huo wa hadhara
Mwenyekiti wa CCM Korogwe Mjini Emanuel Charles akizungumza katika mkutano huo kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Mtera,Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kampeni hizo.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wananchi wa Kata ya Majengo kumchagua mgombea wa CCM ili waweze kushirikiana naye kuhakikisha maendeleo yanapatikana kwa kasi zaidi.
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka wananchi kuhakikisha hawafanyi makosa kwa kumpa kura nyingi za kutosha mgombea udiwani wa CCM kwani dhamira yake ni kuhakikisha anawapatia maendeleo kwa kiwango kikubwa.
Mgombea Udiwani wa Kata ya Majengo katika Halmashauri ya Korogwe Mji kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Mustapha Shengwatu akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Sabasaba sokoni.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga Allan Kingazi katikati akifuatilia hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Mtera mkoani Dodoma Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo kulia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda na kushoto ni Mgombea Udiwani wa CCM Mustapha Shengwatu.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)Mkoa wa Tanga Allan Kingazi kushoto akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani Dodoma (CCM) Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji wakati wa uzinduzi huo katikati anayeshughudia ni Mbunge wa Jimbo la Korogwe Mjini (CCM) Marry Chatanda (Habari kwa hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha)
Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani Dodoma (CCM) Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji akisalimiana na makada wa CCM mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Sabasaba sokoni wakati wa uzinduzi huo kampeni za mgombea Udiwani kupitia chama hicho kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Allan Kingazi
Mbunge wa Jimbo la Mtera Mkoani Dodoma (CCM) Livingstone Lusinde maarufu kama Kibajaji katikati akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM Mkoa wa Tanga kushoto ni Katibu wa CCM Mkoa wa Tanga,Allan Kingazi kulia ni Katibu wa CCM Korogwe Mjini,Ally Issa Ally na Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu wakiingia uwanja wa Sabasaba sokoni tayari kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni za mgombea udiwani wa CCM Kata ya Majengo
Mbunge wa Jimbo la Korogwe Vijijini (CCM) Stephen Ngonyani alimaarufu Proffesa Maji Marefu kushoto akifuatilia kwa umakini hotuba ya Mbunge wa Jimbo la Mtera (CCM) Livingstone Lusinde alimaarufu Kibajaji wakati wa uzinduzi wa kampeni za Udiwani Kata ya Majengo Halmashauri ya Korogwe Mjini huku akiwa na viongozi mbalimbali wa CCM.
Sehemu ya umati wa wananchi wakifuatilia kampeni hizo.
No comments:
Post a Comment