Habari za Punde

MAKAMU WA RAIS AFUNGUA KIKAO CHA KUJADILI CHANGAMOTO ZA MUUNGANO ZINAZOHUSU SEKTA YA FEDHA NA BIASHARA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameongoza kikao kilichuhudhuriwa na Mawaziri kutoka Serikali ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Viongozi wengine ambacho kimejadili changamoto za Muungano zinazohusu sekta ya fedha na biashara katika ukumbi wa ofisi ya Makamu wa Rais ,Luthuli jijini Dar es Salaam. (Picha zote na Ofisi ya Makamu wa Rais)​
 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba akielezea masuala mbali mbali ambayo yamejadiliwa na Mawaziri wa Tanzania Bara pamoja Visiwani.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati)akiongoza kikao cha  Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kushoto ni Waziri wa Nchi Afisi ya Makamo wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed aboud Mohamed na kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.