Habari za Punde

SIMBA WALAZIMISHWA KUNYWA 'ULANZI' UWANJA WA UHURU

 Beki wa Simba, Yusuph Mlipili (kushoto) akijaribu kumdhibiti mshambuliaji wa Lipuli Fc, Ramadhan Mandebe, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Katika mchezo huo timu hizo zimetoka sare ya bao 1-1. Simba ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya 15 kupitia kwa kiungo wake, Mwinyi Kazimoto na dakika tano baadaye Lipuli wakasawazisha kupitia kwa Beki wake Asante Kwasi kwa mpira wa adhabu ndogo.
Beki wa Simba Mohamed Hussein (kushoto) akiwania mpira na beki wa Lipuli Fc, Hussein Rashid, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani (MAFOTO)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.