Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulile akikata
utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara
ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo jijini Dar es salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa
Mafunzo na Rasilimali watu ambae alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
Dkt. Otilie Gowelle.kulia ni Mwenyekiti wa bodi hiyo Dkt Esther Jason.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulile akimkabidhi Mwenyekiti wa Bodi Dkt. Esther Jason mwongozo wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Wapili kushoto ni Mkurugenzi wa Mafunzo na Rasilimali watu ambae alimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Otilie Gowelle.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulile akimkabidhi vitendea kazi Mkemia Mkuu wa Serikali Fidelice Mafumiko wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Dkt. Esther akiongea akitoa neno mbele ya viongozi wa Serikali na Waandishi wa Habari wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulileakisisitiza jambo mbele ya Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mku na viongozi wengine wa Srikali wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu.
Picha ya pamoja ikiongozwa na Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndegulile wakati wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali leo jijini Dar es salaam.
**********************************************
Na WAMJW-DAR ES SALAAM.
SERIKALI kupitia Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeitaka Mamlaka ya Maabara
ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuchukua hatua ya kupima maji yanayotiririka mitaani
kutoka viwandani kubaini kama yana kemikali ambazo zinaathiri wananchi au
hazina madhara yoyote.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa
Afy, Maendeleo ys Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile wakati
wa uzinduzi wa Bodi Tendaji ya Kwanza ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa
Serikali leo jijini Dar es salaam.
"Bodi hii ninayoizindua leo
inatakiwa kuhakikisha majibu ya watu wanaokuja kuleta vipimo vyao yatoke
mapema na haraka iwezekanavyo ili kupunguza msongamano wa wateja wenu"
alisema Dkt. Ndugulile.
Aidha Dkt. Ndugulile amesema kuwa
Mamlaka hiyo inatakiwa kushirikiana na kufanya mazungumzo na Taasisi ya
Chakula na Dawa TFDA na TBS ili kutoingiliana katika majukumu kwani kuna kuna
kipengele cha majukumu yao kinafanana katika kusimamia ubora wa chakula.
Aidha Dkt. Ndugulile ameitaka
Mamlaka hiyo kuisimamia kikamilifu sheria ya uchafuzi wa Mazingira ili kuepusha
wananchi na magonjwa ya kuambukiza na yasioambukiza.
Kwa upande wake Mkemia Mkuu wa
Serikali ambaye pia ni Katibu wa Bodi hiyo Dkt. Fidelis Mafumiko amesema kuwa
wanaiomba Serikali kutatua changamoto ya upungufu wa mitambo ya kufanyia kazi
katika mamlaka hiyo.
Aidha Dkt. Mafumiko amesema kuwa
Bodi hiyo iliyozinduliwa leo ipo tayari kufanya kazi kwa manufaa ya
Watanzania japo mamlka hiyo ina upungufu wa Watumishi kutoka watumishi
400 mpaka kufikia watumishi 220.
Bodi ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia
Mkuu wa Serikali imezinduliwa leo ikiwa na Wajumbe saba ambao ni Mwenyrkiti wa
bodi hiyo Prof. Esther Hellen, Katibu Dkt. Fidelis Mafumiko, Dkt. Eliud
Eliakimu, Dkt. Samwel Gwamaka, Dcp. Hussein Laiser, Bi. Irene Leisure na
Bw. Pius Mponzi
No comments:
Post a Comment