Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), Dkt. Agnes Kijazi (Kkushoto) akiteta jambo na
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Seleman Kakoso, wakati
kamati hiyo ilipotembelea mamlaka hiyo kukagua namna inavyofanya kazi, jijini
Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Elias Kwandikwa, akimsikiliza Kaimu Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi,
Aunyisa Meena (kushoto), kuhusu namna walivyojipanga kuimarisha miundombinu ya
miradi ya hali ya hewa kwa mwaka mpya wa fedha 2018/2019, wakati Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Miudombinu ilipotembelea Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA),
jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Seleman Kakoso (katikati), akifafanua
jambo wakati kamati hiyo ikiwa katika ziara ya kujifunza namna Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA) inavyofanya
kazi, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa.
Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dkt. Agnes Kijazi.
Mkurugenzi Mkuu
wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Nchini (TMA), Dkt. Agnes Kijazi (kulia), akifafanua
jambo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, wakati Kamati hiyo
ilipokuwa kwenye ziara ya kujifunza namna mamlaka hiyo ivyofanya kazi. Katikati
ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Seleman Kakoso na wa kwanza kulia ni Naibu
Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa
Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Seleman Kakoso (katikati), akiwa
na Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (kushoto), katika chumba cha
kutangazia taarifa za hali hewa, wakati kamati hiyo ilipotembelea Mamlaka ya
Hali ya Hewa Nchini (TMA), jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Bi. Hellen Msemo
kutoka Mamlaka hiyo.
No comments:
Post a Comment