Ofisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Bw. Helly Shindano Akimhudumia Dereva wa Pikipiki katika banda la TRA wakati wa Maonesho ya
42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018.
Wanachama wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Wilaya ya Temeke
(UWAPITE) jijini Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya banda la
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakiwa wameshika Namba za Utambulisho wa
Mlipakodi (TIN) wakati wa Maonesho ya 42 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya
mwaka 2018.
Wanachama wa Umoja wa Waendesha
Pikipiki Wilaya ya Temeke (UWAPITE) jijini Dar es Salaam wakiwa katika banda la
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakisubiri kupatiwa huduma ya usajili na
kupewa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) wakati wa Maonesho ya 42 ya
Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018.
Ofisa wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato
Tanzania (TRA), Bi. Jackline Lutare
akisikiliza kero za mteja katika banda la TRA wakati wa Maonesho ya 42
ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) ya mwaka 2018. PICHA ZOTE NA BENEDICT
LIWENGA.
*********************************************
Na Veronica Kazimoto,Dar es Salaam
Madereva wa Bodaboda ambao ni wanachama wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Wilaya ya Temeke (UWAPITE) wamefurahishwa na huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam.
Madereva wa Bodaboda ambao ni wanachama wa Umoja wa Waendesha Pikipiki Wilaya ya Temeke (UWAPITE) wamefurahishwa na huduma zinazotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam.
Madereva
hao wapatao 20 wametembelea banda la TRA kwa ajili ya kusajiliwa na
kupatiwa Namba ya Utambulisho wa Mlipakodi (TIN) kwa lengo la kukatia
leseni mara baada ya kumaliza mafunzo ya udereza wa pikipiki
yaliyotolewa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Temeke kwa kushirikiana
na umoja huo.
Akizungumza baada ya kusajiliwa madereva hao,
Mwenyekiti wa umoja huo Said Kagomba amesema kuwa, amefurahishwa na
huduma nzuri waliyopatiwa na TRA ambapo wanachama wote wamesajiliwa na
kupatiwa na TIN kwa muda mfupi.
"Mimi kama Kiongozi wa Umoja huu
nimefurahia sana huduma tuliyopata hapa TRA, kwanza tumepokelewa vizuri
na kisha tumehudumiwa haraka na kila mwananchama amepatiwa cheti chake
cha TIN na sasa tunaendelea na hatua nyingine ya kwenda kukata leseni,"
alisema Kagomba.
Naye mmoja wa Madereva hao Ramadhan Mwilombwa
ametoa wito kwa vijana kujiunga katika vyama mbalimbali kwa kuwa kuna
faida nyingi ikiwa ni pamoja na kupata mafunzo, TIN na leseni kwa
urahisi kwa sababu viongozi wa vyama husika wanajua sheria na taratibu
mbalimbali. "Ninaomba vijana wenzangu wajiunge
na vyama hivi kwa sababu palipo na wengi hakiharibiki kitu. Mimi
binafsi mpaka sasa nimepata faida nyingi za kujiunga na Umoja huu,
kwanza nimepata mafunzo ya udereva na kujua vizuri sheria za barabarani,
pili nimefahamiana na vijana wenzangu ambao nilikuwa siwafahamu hivyo
nimeongeza marafiki, tatu nimefanikiwa kusajiliwa na TRA na kupata TIN
na mwisho kiongozi wetu ametuambia tunakwenda kukata leseni," alifafanua
Mwilombwa.
Mamlaka ya Mapato Tanzania inaendelea kutoa huduma
mbalimbali katika Maonyesho ya Sabasaba. Miongoni mwa huduma hizo ni
pamoja na kusajili walipakodi, kuelimisha wananchi umuhimu wa kulipa
kodi, kutoa bili na kulipa Kodi ya Majengo.
Huduma nyingine ni
kuelezea haki na wajibu wa Mlipakodi kama ilivyoainishwa katika Mkataba
wa Huduma na Mlipakodi, kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya mashine za
Kielektroniki za kutolea Risti (EFDs), kuelezea mwenendo wa makusanyo
ya mapato ya Serikali, na kupokea maoni, malalamiko, mrejesho pamoja na
mapendekezo mbalimbali kutoka kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment