Habari za Punde

MATUKIO KATIKA PICHA YANGA ILIPOLALA BAO 1 KWA SIMBA TAIFA JANA


Kipa wa Simba Aishi Manula akiokoa moja ya hatari langoni kwake mpira uliopigwa na Herietier Makambo (kushoto) wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Simba walishinda bao 1-0.
Mshambuliaji  wa Yanga, Mohamed Issa 'Mo Banka' (kushoto,) akijaribu kuwatoka mabeki wa Simba, Mohamed Hussein (katikati) na Hassan Dilunga, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.  
  MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mrisho Ngassa, (kushoto) akimtoka beki wa Simba, Mohamed Hussein, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Mkude (kulia) akimtoka Ibrahib Ajib
  Dante akimdhibiti Kagere
Beki wa Simba, Mohamed Hussein, akijaribu kutako kumzuia beki wa Yanga,, Paulo Godfrey, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
 Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Ibrahim Ajib, akijaribu kuwatoka mabeki wa Simba, Pascal Wawa na Jonas Mkude, wakati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam
 Heka heka langoni mwa Simba
 Mashabiki wa Simba wakicheza kiduku kwa furaha

Wachezaji wa Yanga wakipasha kabla ya mchezo huo
 Wachezaji wa Simba wakipasha kablla ya mchezo huo
 Mashabiki wakiingia aauwanjani
 Makomandoo wa SImba wakiwazuia waandishi wa habari kuingia ndani kwa kutumia mlango wao baada ya wao kulazimisha kuwapitisha wachezaji kupitia mlango huo kinyume na taratibu
 Fursa za biashara pia zilikuwepo mahala hapo
 Mwanadada akipita na biashara yake ya Maziwa ya mtindi katika jukwaa la Simba
 Huku nje mwanadada huyu nae akiuza vuvuzela huku akitumia staili ya Kagere ya kuziba jicho moja.
 Katika jukwaa la Simba zilianza mapema 
 Shabiki wa Yanga akikatiza mitaa wakati akielekea uwanjani
 Askari Polisi akiwatimua mashabiki waliokuwa wameketi jukwaa lisilo lao kinyume na utaratibu

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.