Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Nicholas Mkapa, (wa pili kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Upimaji Ardhi ya Gromaps Africa Ltd, Joseph Tairo, kuhusu vifaa vya upimaji ardhi wakati alipofika kufungua Mkutano mkuu wa mwaka 2019 na Kongamano la Chama cha Wapima Ardhi Tanzania (IST) uliofanyika jijini Dar esc Salaam, leo. Kushoto ni Makamu wa Rais wa hicho, Bille Mussa. (Picha Zote na Muhidin Sufiani).
Makamu wa Rais wa Chama hicho, Bille Mussa, akijaribu kufafanua jambo kwa Naibu Katibu Mkuu huyo.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Nicholas Mkapa, (wa tatu kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Upimaji Ardhi ya Global Sarvay Ltd, Daud Msungu, kuhusu vifaa vya upimaji ardhi wakati alipofika kufungua Mkutano mkuu wa mwaka 2019 wa Chama cha Wapima Ardhi Tanzania (IST) uliofanyika jijini Dar es Salaam, leo sambamba na Kongamano.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Nicholas Mkapa, (wa tatu kulia) akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Mradi wa Kampuni ya Cosmomaps Consult Ltd, Khatibu Semkieti, kuhusu vifaa vya vinavyotumiwa na wapimaji ardhi wakati alipofika kufungua Mkutano mkuu wa mwaka 2019 wa Chama cha Wapima Ardhi Tanzania (IST) uliofanyika jijini Dar es Salaam, leo sambamba na Kongamano.
Mshiriki wa Kongamano hilo akipitia maandiko.
Washiriki wakisikiliza kwa makini.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Nicholas Mkapa, akizungumza wakati akifungua Mkutano mkuu na Kongamano la mwaka 2019 la Chama cha Wapima Ardhi Tanzania (IST) uliofanyika jijini Dar esc Salaam.
********************************************************
SERIKALI kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, imewataka wadau wa ardhi kutoa maoni ya sheria zilizopitwa
na wakati ili ziweze kufanyiwa marekebisho mara moja.
Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
hiyo,Nicholas Mkapa kwa niaba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Wiliam Lukuvi wakati wa ufunguzi wa kongamano la wapimaji ardhi Tanzania
na Mkutano Mkuu wa mwaka wa IST uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mkapa alisema serikali imekuwa ikitunga sheria na
kanuni ili ziweze kutoa dira ya kiutendaji
na kusimamia utendaji wa wana taaluma husika.
“Natambua kuwa taaluma ya upimaji na ramani nchini inaongozwa na sheria mbili yaani CAP324 ordinance law na Sheria namba
mbili ya mwaka 1977,hizi za zamani na zimepitwa na wakati hivyo zinahitaji
kufanyiwa marekebisho ili ziweze kuendana na wakati,” alisema.
Alisema sasa taaluma ya upimaji imekuwa,teknolojia
na uandaaji wa ramani umekuwa ukibadilika kwa kiwango kikubwa na kusababisha
sheria hizo kuwa kikwazo cha maendeleo ya taaluma hiyo.
“Wizara yangu imetoa maelekezo kwa wadau wote kutoa
maoni ili sheria hizo zifanyiwe marekebisho na nimemuelekeza mkurugenzi wa
upimaji ramani kuwashirikisha wadau wote
kutoa maoni ili kuweza kupata sheria itakayokidhi mahitaji,matumaini yangu
mchakato huu utaharakishwa ili marekebisho yafanyike mapema na kuendana na kasi
ya serikali katika utekelezaji wa
majukumu yenu,”alisema. KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Vilevile Mkapa alisema wizara hiyo kwa kushirikiana
na watamu wa kimataifa imeshakamilisha kazi ya kuunda mfumo mpya wa upimaji
utakaotumika kwa ajili ya kazi zote za upimaji ardhi.
Alisema
mfumo huo unaendana na unatumika kimataifa
ambao unatumia taarifa zilizoboreshwa kuhusu ukubwa na umbo la dunia.
Mkapa alisema mfumo huo umekamilika na unatarajiwa
mwishoni mwa mwaka kuchapishwa kwenye
gazeti la serikali.
Pia ameitaka IST kuweka mkakati maalumu wa kujenga
utaratibu wa kudhibiti maovu kwa taaluma
hiyo ili kuweza kutoa ushirikiano wa
kutosha kwa serikali na kutoa msaada wa ufafanuzi wa mwenendo wa taaluma na watalamu wa upimaji.
RAIS
WA IST
Makamu wa Rais wa Chama cha Wapimaji Ardhi Tanzania, Bille Mussa, akizungumza katika mkutano huo kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi.
Naye Rais wa Chama cha Wapimaji Ardhi Nchini(IST)
Bille Mussa alisema mkutano huo umewakutanisha wataalamu wa upimaji ardhi 130
na kampuni tano ambazo mbili zimefadhili mkutano na tatu zimeshiriki maonesho.
Alisema
lendo la mkutano huo ni kukidhi matakwa ya kikatiba ya chama hicho,kujadili
changamoto za kitaalamu na kuangalia
muelekeo wa taaluma ili kujenga uwezo juu ya teknolojia inayobadilika kila
siku.
Mussa alisema mkutano huo umebebwa na kauli mbiu ya
upimaji ardhi na maendeleo endelevu katika sekta ya ardhi mafanikio na
changamoto zake.
Hata hivyo aliiombna wizara hiyoi kuharakisha
marekebisho ya sheria zilizopitwa na wakati
na kuendeleza ushirikiano uliopo kwa manufaa ya watanzania.
WADAU
WANENA
Naye mwalimu
wa Upimaji wa Ardhi, Joseph Tairo alitaja changamoto inayoikumba taaluma hiyo
ni ajira hivyo aliiomba wizara kuangalia
namba ya kuweza kuwaajiri wanataaluma kwani wanahitajika sana kwa
maendeleo ya taifa.
“Kikubwa wapimaji ardhi waajiriwe kwani wengi wao wamemaliza masomo na kufanya
kazi kwenye taasisi au kampuni tofauti na walichokisomea,hivyo ni vyema mfumo
wa ajira ukaangaliwa kwa namna yake,”alisema.
Naye Mpima Ardhi Kanda ya Kaskazini,Nina Rutakyamirwa
ambaye ni ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza kwenye taaluma hiyo mwaka1992,aliwahimiza
wanawake kutoiogopa fani hiyo kwani haina toifauti na ya uhandisi.
Mkono wa pongezi kwa wadau
Mkono wa pongezi kwa wadau
Mkono wa pongezi kwa wadau
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Nicholas Mkapa, (katikati) akimkabidhi cheti cha shukrani Mpimaji Ardhi Godwin Saiguran, wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka 2019 na Kongamano la Chama cha Wapima Ardhi Tanzania (IST) uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Nicholas Mkapa, (wa pili kushoto) akimkabidhi cheti cha shukrani Mpimaji Ardhi wa Chuo cha Madini Dodoma, Sunday Brown, wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa mwaka 2019 na Kongamano la Chama cha Wapima Ardhi Tanzania (IST) uliofanyika jijini Dar es Salaam,
Cheti cha shukrani
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja
Ujumbe maalumu.
No comments:
Post a Comment