Habari za Punde

TAIFA STARS YAWASHA MOTO NYUMBANI YAIPA GUINEA 2-1

 Winga wa timu ya Taifa Taifa Stars, Simon Msuva, akibinjuka Sarakasi hewani kushangilia bao lake la kusawazisha alilofunga kipindi cha pili wakati wa mchezo wa kuwania kufudhu Afcon 2021 uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam jana dhidi ya Equatorial Guinea. Katika mchezo huo Taifa Stars ilishinda mabao 2-1. (Picha Zote na Muhidin Sufiani).
 Mshambuliaji wa timu ya Taifa Taifa Stars, Mbwana samatta , akijaribu kupiga shuti mbele ya beki wa Equatorial Guinea,Pedro Mba Obiang, wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2021 uliochezwa katika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
 Winga wa timu ya Taifa Taifa Stars, Farid Mussa, akimiliki mpira mbele ya mabeki wa Equatorial Guinea,  wakati wa mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2021 uliochezwa katika Uwanja wa Taifa. 
 Samatta, akibanwa na wachezaji wa Guinea
 Samatta akipiga kichwa mpira wa krosi na kukosa bao
 Farid Mussa, akiwania mpira na beki wa Guinea
 Faridi Mussa, akimfinya beki wa Guinea, CarlosAkapo Martnez
 Faridi Mussa, akimtoka beki wa Guinea, CarlosAkapo Martnez
 Farid Mussa (kulia) akijiandaa kupiga krosi mbele ya beki wa Equatorial Guinea, CarlosAkapo Martnez, 
 Mshambuliaji wa Taifa Stars, Betram Nchimbi, akimiliki mpira huku akizongwa na mabeki wa Guinea.
 Raha ya mechi, Bao, Msuva na Faridi wakishangilia bao la kusawazisha. 
 Mfungaji wa bao la pili, Salum Abubakar 'Sure Boy', akijaribu kuwahadaa mabeki wa Guinea
 Winga wa timu ya Taifa Taifa Stars, Simon Msuva (kushoto) akimtoka beki wa Equatorial Guinea, Basilio Ndong Owono Nchama.
 Mohamed Hussein akimbeba Sure Boy kumpongeza kwa bao alilofunga.
 Wachezaji wa Guinea na viongozi wakifoka na kumlaumu mwamuzi wakijaribu kuingia uwanjani baada ya mchezo kumalizika. 
 Stars wakiomba dua baada ya mchezo kumalizika
 Wakitoka nje
 Sehemu ya mashabiki waliohudhulia mechi hiyo wakishangilia.
 Kelvin Yondani akipeana tano na Hassan Dilunga
 Mashabiki wakiwapongeza Samatta na Msuva baada ya mchezo kumalizika.
 Mashabiki wakiwapongeza Samatta na Msuva baada ya mchezo kumalizika.  
Msanii wa Muziki wa Singeli, Dullah Makabila, akiimba sambamba na wanenguaji wake wakati wakitoa burudani katika mchezo wa Kimataifa kati ya Taifa Stars na Equatorial Guinea, katika Uwanja wa Taifa.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.