Habari za Punde

KITUO CHA MSAADA WA SHERIA WLAC CHAZINDUA KAMPENI YA USAWA WA KIJINSIA

 Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake WLAC, Wakili Theodosia Muhulo, akizungukmza na waandishi wa habari katika Ofisi za Kituo hicho jijini Dar es Salaam, leo wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Kampeni ya Usawa wa kijinsia kwa Maendeleo ya Jamii, Ajira sawa na Ujira sawa kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayosherehekewa kesho. Katikati ni mmoja kati ya mashuhuda wa vitendo vya unyanysaji, Hellen Kayanza na Rehema Mathias. (Picha na Muhidin Sufiani)
************************************************
KAMPENI hiyo iliyozinduliwa leo yenye lengo la kuelimisha jamii kuhusu Usawa katika sekta ya ahira na kusaidia Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu ili kutambua haki zao katika maeneo ya kazi, imedfadhiliwa na Shirika la  Legal Services Facility (LSF).
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Kituo hicho jijini Dar es Salaam, leo Mkurugenzi Mku wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake WLAC, Wakili Theodosia Muhulo, amesema kuwa kuelekea maadhimisho ya siku hiyo maalumu ya Wanawake Duniani, pia ni fursa kwa Taifa kuweza kutafakari juu ya usawa wa jinsia katika kuleta maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Aidha aliongeza kuwa pamoja na kuwepo uwiano sawa katika nyanja zote za kiuchumi,kisiasa na kijami. Wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika biashara, kilimo, ujasiriamali au wafanyakazi ajira rasmi na zisizo rasmi au kupitia kazi za nyumbani ambazo mara nyingi jamii hazioni kama mchango mkubwa kwa uchumi wa Taifa.
Aliongeza kuwa ili kuhakikisha kuwa wanawake wanaweza kuchangia kikamilifu na kufaidika kiuchumi, Serikali imeweka sheria mbalimbali zenye usawa na fursa za wanawake katika uchumi kama vile sheria za Ardhi za mwaka 1999 zinazotoa fursa kwa wanawake na wanaume katika kupata, kutumia na kumiliki  ama kufaidika na ardhi. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeweka bayana, usawa bila kujali jinsia na kupinga vitendo vyote vya ubaguzi.
''Licha ya kuwepo na sera na sheria zenye mtazamo wa kijinsia lakini bado kuna mila na desturi kandamizi kwa wanawake na watoto hususan watoto wa kike, hivyo basi jamii inatakiwa kubadili mtazamo nakutoa ulinzi kwa wanawake na watoto ili waweze kuishi salama bila ukatili, kwa sababu Jamii bila ukatili wa kijinsia inawezekana''. alisema Wakili Theodosia
 Mkurugenzi wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake WLAC, Wakili Theodosia Muhulo (katikati) akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa kituo hicho wakiwa na vipeperushi vya uzinduzi wa Kampeni ya Kampeni ya Usawa wa kijinsia kwa Maendeleo ya Jamii, Ajira sawa na Ujira sawa kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani inayosherehekewa kesho.
 Wakifurahia jambo
 Ofiasa habari wa Kituo hicho, Consolata akifafanua jambo
 Baadhi ya wafanyakazi wa Kituo hicho wakishuhudia tukio hilo.
 Baadhi ya kina mama na mashuhuda wa vitendo vya ukatili na unyanyasaji waliohudhuria uzinduzi huo.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.