Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
Mhe. Dkt. Selemani Jafo amewasilisha Bungeni Mapitio ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti kwa mwaka 2021/22
na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2022/23.
Akiwasilisha hotuba hiyo leo Aprili
27, 2022, Dkt. Jafo amesema Ofisi ya Makamu wa Rais itaendelea kuratibu utatuzi wa
changamoto za Muungano zilizobakia na zitakazojitokeza katika utekelezaji wa
masuala ya Muungano kupitia Vikao vya
Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ya Kushughulikia Masuala ya Muungano.
Aidha, Waziri Jafo alisema Ofisi
itaendelea kuratibu Masuala ya Kiuchumi na Kijamii; Kuratibu masuala yasiyo ya Muungano kupitia vikao vya
ushirikiano vya Wizara, Idara na Taasisi za SJMT na SMZ zisizo za Muungano
zenye majukumu yanayoshabihiana; kutoa elimu kwa Umma kuhusu Muungano na kuratibu
utekelezaji wa masuala 22 ya Muungano.
Aliongeza kuwa katika kuhakikisha
hifadhi endelevu ya mazingira, kwa mwaka 2022/23, Ofisi imepanga kutekeleza
vipaumbele sita ambavyo ni kuratibu utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Mazingira
ya Mwaka 2021; kuratibu utekelezaji wa Mpango Kabambe wa
hifadhi ya Mazingira na kufanya mapitio ya Sheria ya Usimamizi wa
Mazingira, Sura 191.
Vipaumbele vingine ni kuratibu utekelezaji wa
Kampeni Kabambe ya Hifadhi na Usafi wa Mazingira; kuendelea kujenga uwezo kwa
jamii katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya Tabianchi na kuendelea
kutoa elimu kwa umma kuhusu Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira.
Baada
ya michango mbalimbali ya wabunge Bunge limeidhinisha makadirio ya jumla ya Sh. 53,116,317,000
kwa mwaka wa
fedha wa 2022/23.
No comments:
Post a Comment