Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna (katikati) na Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya Nmb, Filbert Mponzi (kulia) wakipeperusha Bendera za NMB kuashiria kuzindua rasmi wa Kampeni ya kuinadi Kampeni ya TELEZA KIDIJITALI kwa Mkoa wa Dar es Salaam, iliyofanyika katika Tawi la Benki ya NMB Tandika jijini Dar es Salaam, Katika Kampeni hiyo Wafanyakazi wa NMB walitembelea mitaani na kutoa elimu kwa wateja kuhusu mikopo ya Mshiko Fasta, Lipa Namba na NMB Pesa Wakala na kufungua Akaunti.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, akizungumza wafanyabiashara wa duka la Vipodozi, Hamede Shirima (katikati) na Haruna Masoud, wakati walipokuwa wakitembea mitaani kuinadi Kampeni ya TELEZA KIDIJITALI kwa Mkoa wa Dar es Salaam, iliyofanyika katika Tawi la Benki ya NMB Tandika jijini Dar es Salaam, Katika Kampeni hiyo Wafanyakazi wa NMB walitembelea mitaani na kutoa elimu kwa wateja kuhusu mikopo ya Mshiko Fasta, Lipa Namba na NMB Pesa Wakala na kufungua Akaunti.
BENKI
ya NMB imeanza rasmi kuinadi Kampeni ya Teleza Kidijitali iliyozinduliwa Aprili
11 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jijini Dodoma, na sasa ikipelekwa mtaani, kuwaelimisha
wateja na wasiokuwa wateja umuhimu wa huduma zilizo chini ya mwamvuli huo,
ambazo ni NMB Pesa Wakala, Lipa Namba na Mshiko Fasta.
Uzinduzi
huo kampeni hiyo umefanyika NMB Tawi la Tandika Wilayani Temeke jijini Dar es
Salaam, ambako Ofisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, aliambatana na Afisa
Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi na Meneja wa NMB Kanda ya
Dar es Salaam, Donatus Richard, kuzindua na kisha kuwatembelea wafanyabiashara
madukani kuwapa elimu.
Akizungumza
baada ya uzinduzi huo, Zaipuna alisema ujio wake yeye na viongozi wengine
waandamizi wa NMB Makao Makuu, kuungana na wale wa Tawi la Tandika, umelenga
kutoa elimu ya kutosha na kuwaingiza Watanznaia kwenye Sekta Rasmi ya Kifedha
ili waweze kunufaika na huduma mbalimbali ambazo wanazitoa.
“Tuko
hapa kunadi huduma zote muhimu zilizo kwenye mwamvuli wa Teleza Kidijitali,
ambazo ni Mshiko Fasta ambayo ni mikopo nafuu isiyo na dhamana, inayopatikana
kwa njia ya simu kwa wateja wenye akaunti, ambako mteja ahitaji kitambulisho
wala dhamana yoyote kuupata.
“Pia
tumeutumia uzinduzi na kampeni hii kwa ujumla kunadi huduma ya Lipa Namba,
ambayo itamuwezesha mfanyabiashara kuitumia kulipwa kwa namba na wateja wake, huku
ikitupa sisi kumbukumbu na historia ya mfanyabiashara ambaye ni mteja wetu
kihuduma na kujua levo ya uaminifu na utumiaji wa huduma zetu.
“Pia
tumekuja na NMB Pesa Wakala, huduma inayomuwezesha mtu yeyote kuwa wakala bila
kutumia mashine, ambayo itamuwezesha kutoa huduma za kuweka, kutoa ama kutuma
pesa kirahisi kwa kutumia hata simu ya kitochi,” alisema Zaipuna, ambaye
alishiriki kutembelea wafanyabiashara wa eneo la Tandika madukani mwao kutoa
elimu na kusikiliza maoni yao.
Zaipuna
aliielezea kampeni hiyo kwamba imelenga kuhakikisha wanawapa elimu Watanzania
waweze kuwa sehemu ya watumiaji wa huduma za sekta rasmi kifedha na kwamba
wanaamini NMB Pesa Wakala, Lipa Namba na Mshiko Fasta, vitakuwa chachu ya
ukuaji kibiashara na kiuchumi kwa wateja wao kot, ambako wameahidi
kuifikisha Teleza Kidijitali.
Kwa
upande wake, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, aliwataka
wakazi wa kanda yake kuchangamkia Teleza Kidijitali, ili kurahisisha
upatikanaji wa huduma bila kusumbuka kwenda matawini, ili kuokoa muda wa
kufanya shughuli nyingine za kukua kiuchumi.
“Wito
wangu kwa wakazi wa Kanda yangu ya Dar es Salaam, inayojumuisha Zanzibar na
mkoa wa Pwani, ni vema wanapofikiria kufungua akaunti, wafanye hivyo na Benki
ya NMB, ambako watapata manufaa makubwa na masuluhisho mbalimbali ya kiduma na
tutakuwa sehemu ya ustawi wao kibiashara na kiuchumi,” alisistiza Donatus.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, akizungumza Mfanyabiashara wa vitambaa, Julius John (kulia), wakati walipokuwa wakitembea mitaani kuinadi Kampeni ya TELEZA KIDIJITALI kwa Mkoa wa Dar es Salaam, iliyofanyika katika Tawi la Benki ya NMB Tandika jijini Dar es Salaam, Katika Kampeni hiyo Wafanyakazi wa NMB walitembelea mitaani na kutoa elimu kwa wateja kuhusu mikopo ya Mshiko Fasta, Lipa Namba na NMB Pesa Wakala na kufungua Akaunti. Kushoto kwake ni Meneja Tawi la NMB Tandika, Jacob Jacob.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna, akizungumza Mfanyabiashara wa vitambaa, Juma Hamad (kulia), wakati walipokuwa wakitembea mitaani kuinadi Kampeni ya TELEZA KIDIJITALI kwa Mkoa wa Dar es Salaam, iliyofanyika katika Tawi la Benki ya NMB Tandika jijini Dar es Salaam, Katika Kampeni hiyo Wafanyakazi wa NMB walitembelea mitaani na kutoa elimu kwa wateja kuhusu mikopo ya Mshiko Fasta, Lipa Namba na NMB Pesa Wakala na kufungua Akaunti.
No comments:
Post a Comment