Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe, akishikana mkono na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, ikiwa ni ishala ya makabidhiano ya jumla ya madawati 100 yaliyotolewa na benki hiyo kwa Shule ya Msingi Msasani, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika shuleni hapo, ambapo pia walikabidhi vifaa vya Hospitali kwa ajili ya Zahanati ya Madale iliyopo Tegega jijini Dar es Salaam, vyote vikiwa na thamani ya Sh milioni 16. Wengine pichani ni baadhi ya Viongozi wa Chama na Serikali na walimu waliohudhuria hafla hiyo. Picha zote na Muhidin Sufiani
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe, akipokea sehemu ya vifaa vya Hospitali kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa hivyo vilivyotolewa na benki hiyo kwaajili ya kusaidia wagonjwa na wazazi katika Zahanati y Madale iliyopo Tegeta jijini Dar Es Salaam. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika Shule ya Msingi Msasani, ambapo pia walikabidhi jumla ya madawati 100 vyote vikiwa na thamani ya Sh. milioni 16. Wengine pichani ni baadhi ya Viongozi wa Chama na Serikali na walimu waliohudhuria hafla hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, akizungumza wakati wa hafla hiyo
Mkuu wa Wilaya Godwin Gondwe akiwasili shuleni hapo na kusalimiana na baadhi ya viongozi.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe akisalimiana na Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Donatus Richard, baada ya kuwasili shuleni hapo.
Kilimo : Wakulima wa zao la Ngano Walilia Soko , Wilayani Monduli.
-
Na Jane Edward, Arusha
Wakulima wa zao la ngano wilayani Monduli, mkoa wa Arusha, wameiomba
serikali iwasaidie kuwatafutia soko la jumla ili waweze kunuf...
55 minutes ago
No comments:
Post a Comment