Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Al Had Mussa (wa tatu kulia) akizindua rasmi mbio za Ocean City Community Season 2, wakati wa hafla ya uzinduzi huo iliyofanyika katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam leo. Wa pili (kulia) ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Property International Limited , George Obado na mmoja kati ya waratibu wa mbio hizo. Kushoto ni baadhi ya viongozi kutoka Kampuni ya Property International na baadhi ya waratibu wa mbio hizo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi, mratibu Franklin Tisa, alisema kuwa baada ya kufanikiwa kufanyika mbio za mwaka jana na washindi kukabidhiwa zawadi zao za Viwanja vyenye hati, mbio za mwaka huu zinatarajia kufanyika mnamo tarehe 31 mwezi wa 12 ambapo mshindi wa kwanza atapata zawadi ya Gari aina ya Passo New Model kwa mshindi wa kiume na kike.
Wakifurahia na kupiga makofi baada ya kuzindua rasmi....
Mwanasheria wa Kampuni ya Property International Limited, Hazel Chonya (wa pili kulia) akimkabidhi Hati ya Kiwanja Robert Chacha mzazi wa mtoto Norman Chacha (13) ambaye ni mshindi wa mbizo za Ocean City Community zilizofanyika mwaka jana. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam, leo. Katikati ni Afisa Mwendeshaji Mkuu wa Property International, George Obado , (wa tatu kulia ni Mratibu wa Mbio hizo, Franklin Tisa na msadizi wake, Doris Thomas (kulia)
Mratibu wa Mbio za Ocean City Community Marathon Season 2, Franklin Tisa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio hizo uliofanyika katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni msadizi wake, Doris Thomas.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Al Had Mussa, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa hafla ya uzinduzi wa mbio za Ocean City Community Marathon Season 2 uliofanyika katika Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Mratibu wa mbio hizo msadizi wake, Doris Thomas.
Mgeni rasmi Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Al had Mussa, na baadhi ya viongozi wakijaribu kuigiza kukimbia mbio za marathon baada ya kuzindua rasmi mbio hizo za mwaka huu kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es Salaam, leo.
No comments:
Post a Comment