Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akizungumza na wataalamu, watafiti na wanasayansi wa rasilimali za bahari wakati alipokuwa akifungua warsha ya uhakiki wa taarifa ya upembuzi yakinifu wa awali kuhusu mpango wa matumizi ya maeneo ya bahari (MSP) kwa Nchi za Magharibi mwa bahari ya Hindi iliyoandaliwa na Serikali ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kwa kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais. Kongamano hilo lilifunguliwa leo
.....................................................................
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga ametoa wito kwa watafiti, wataalamu na wanasayansi ya bahari kujadili kwa pamoja namna bora ya kutunza, kusimamia na kuwekeza katika rasilimali za bahari zilizopo nchini ili kuongeza mchango wake katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Ametoa wito huo leo Machi 27, 2023) jijini
Dar es Salaam wakati akifungua Warsha
ya Uhakiki wa Taarifa ya Upembuzi yakinifu wa awali kuhusu Mpango wa Matumizi
ya Maeneo ya Bahari (MSP) kwa Nchi za Magharibi mwa Bahari ya Hindi
iliyoandaliwa na Serikali ya Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kwa
kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Bi.
Maganga amesema kuwepo kwa mpango shirikishi wa matumizi ya maeneo ya bahari ni
sehemu ya suluhisho la kuleta matumizi endelevu ya rasilimali za bahari na
kufungua fursa za kiuchumi na ajira kwa kuzingatia utunzaji sahihi wa mazingira
na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
“kuna
fursa nyingi katika matumizi ya Bahari ambazo zikifanyika kwa namna endelevu
zitachangia katika ukuaji wa Uchumi. Shughuli kama vile uvuvi mdogo, uvuvi wa
bahari kuu, ufugaji samaki na mazao ya baharini zina mchango mkubwa katika
kukuza uchumi wa Buluu na hatimaye kukuza uchumi wa nchi” amesema Bi. Maganga.
Aidha
ameeleza kuwa Malengo ya Umoja wa Mataifa hasa lengo Namba 14 la Maendeleo
Endelevu linasisitiza matumizi endelevu ya bahari, ambapo lengo hilo linakwenda
sambamba na malengo ya warsha hiyo inayohimiza kupitia na kuhakiki taarifa ya
upembuzi yakinifu wa awali wa Mpango wa Matumizi ya Maeneo ya Bahari.
Akifafanua
zaidi Maganga amesema kuwa Mpango huo umekuja katika wakati mwafaka ambapo
Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)
kwa kushirikiana na Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar zikiwa
zimejipanga katika kupanua wigo wa matumizi endelevu ya bahari na rasilimali
zake ili ujenga uchumi imara.
Ameongeza
kuwa mafanikio ya Uchumi wa Buluu yanategemea uwepo kwa Mpango Mahsusi wa Matumizi
ya Maeneo ya Bahari, hivyo Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)kwa
kushirikiana na Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi Zanzibar zitaendelea
kushirikiana na wadau katika kuratibu na kushiriki katika utekelezaji wa Mpango
huo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la The Nature Conservancy
kutoka Ujeruamani Bi. Lucy Maghembe amesema washa hiyo imewakutanisha wadau
mbalimbali wa masuala ya sayansi ya bahari waliokutana kwa ajili ya kujadili
sera na mipango endelevu ya usimamizi wa rasilimali za bahari na namna bora ya
kushughulikia migongano ya matumizi ya rasilimali za bahari.
“Katika Afrika Tanzania tunakuwa taifa la nne kuwa na Mpango wa aina hii.
Mataifa mengine ya Kenya, Shelisheli na Mauritius zimeanza utekezaji wa Mpango
huu. Tumejipanga kuja na sera na mipango imara itakayosaidia usimamizi endelevu
wa rasilimali za bahari katika ukanda wa bahari ya Hindi.
Naye Mtaalamu wa Sayansi ya Bahari, Profesa Yunus Mgaya amesema wa
wanasayansi umebaini kuongezeka kasi ya matumizi ya rasilimali za bahari katika
Ukanda wa Bahari ya Hindi hatua inayochangiwa kwa kiasi kikubwa na kuongezeka
kwa shughuli za kijamii na kiuchumi ikiwemo nishati, gesi, utalii n.k
“Utafiti uliofanyika umetoa mapendekezo ya kuwa na mifumo ya kitaasisi inayosaidia
usimamizi na uhifadhi endelevu wa rasilimali za bahari ili kuweza kuzuia
migogoro na migongano baina ya watumiaji wa rasilimali zilizopo baharini”
amesema Prof. Mgaya.
Mkurugenzi Idara ya Uratibu wa Uchumi wa Buluu, Wizara ya Uchumi wa Buluu
na Uvuvi Zanzibar, Zahor Alharousy amesema kupitia Mpango huo uliobuniwa na
wataalamu utaiwezesha Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupanua wigo na fursa za ukuaji
wa uchumi kwa wananchi hususani wavuvi na wakulima wa zao la mwani.
Tumejipanga kikamilifu kuhakikisha Mpango unaondaliwa unakuja na mipango
endelevu ya matumizi ya rasilimali za bahari na kuibua fursa kwa wakulima na
wavuvi"
Warsha hiy imeandaliwa na Shirika la The Nature Conservancy (TNC) kutoka
Nchini Ujeremani inashirikisha wadau, wafadhili na mashirika ya kimataifa
yanaohusika katika usimamizi, matumizi na uwekezaji katika fukwe za
bahari, maziwa na mito.
1. Jumatatu Machi 27, 2023 Jijini Dar es Salaam.
2. Jumatatu Machi 27, 2023 Jijini Dar es Salaam.
3. Jumatatu Machi 27, 2023 Jijini Dar es Salaam.
4. Jumatatu Machi 27, 2023 Jijini Dar es Salaam.
5.
6.
No comments:
Post a Comment