Habari za Punde

RC KUNENGE APOKEA KILIO CHA WANAOTUMIA MABASI YA MWENDO KASI KITUO CHA KIBAHA BUS TERMINAL

WANANCHI wanaotumia usafiri wa mabasi ya Mwendo Kasi (DART) kwenye kituo cha mabasi Kibaha Mkoani Pwani, (Kibaha Bus Terminal) wametoa malalamiko yao kwa  Mkuu Mkoa wa Pwani Mhe. Alhaj Aboubakar Kunenge ya kwamba inawachukua muda mrefu kupata usafiri huo.

RC Kunenge alitembelea kituo hicho Mei 2, 2023 katika utaratibu wake wa kawaida wa kutembelea maeneo yanayotoa huduma za kijamii ili kusikilzia kero au changamoto zinazojitokeza katika utoaji huduma.

Baada ya kupokea kero hiyo RC Kunenge alichukua hatua papo hapo kwa kuwasiliana na uongozi wa juu wa DART ambao nao walimuahidi kuchukua haua za haraka

“Viongozi wa DART wameahidi kufika kwenye kituo hiki lakini pia kuongeza idadi ya mabasi yatakayokuwa yakitoa huduma kati ya Kibaha na Dar es Salaam.” Alifafanua.

Aidha RC Kunenge pia ameelezwa kuwa vibanda vya kujikinga na jua au mvua havijitoshelezi kwenye kituo hicho hususan kwenye eneo la mabasi ya mwendo kasi na mabasi madogo ya abiria.

“ Nia ya Mhe Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan, na sisi wasaidizi wake ni kusikiliza na kutatua kero za wananchi na kuhakikisha upatikanaji wa huduma mbalimbali za kijamii unakuwa rafiki wakati wote.” Aliwahakikishia wasafiri hao.

Mkuu huyo wa Mkoa pia alijionea jinsi Kituo hicho kilivyoathiriwa na mvua ambapo kumekuwa na mashimo.

“Nimewaagiza wataalma wa Halmshauri washirikiane na TANROADS na TARURA kufanya matengenezo ya maeneo yaliyoharibika, lakini pia kuhakikisha vikinga jua vinafanyiwa maboresho haraka.” Alisisitiza RC Kunenge.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.