Habari za Punde

BENKI YA NMB YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO VYA MIL. 16.7 KWA TIMU ZA MAJESHI TANZANIA BAMMATA

Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Aikansia Muro, (katikati) akimkabidhi sehemu ya Tracksut za michezo, Mwenyekiti wa Kanda ya Ngome, Kanali Robert Mbuba, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya Tsh. Milioni 16.7 kwa ajili ya timu za Majeshi zinazo shiriki michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) yanayotarajia kuanza mwezi wa Julai na Agost mwaka huu. (wa pili kulia) ni Meneja Mwandamizi wa Mikopo NMB, Ally Ngingite na Meneja Mwandamizi Idara ya Wateja Binafsi NMB, Isaac Mgwassa (kushoto) ni Kamishna Mdaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zima moto, Laizer Loshipay. 
Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Aikansia Muro, (katikati) akimkabidhi sehemu ya Tracksut za michezo, Mwenyekiti wa Kanda ya Ngome, Kanali Robert Mbuba, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya Tsh. Milioni 16.7 kwa ajili ya timu za Majeshi zinashiriki michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) yanayotarajia kuanza mwezi wa Julai na Agost mwaka huu. (kulia) ni Meneja Mwandamizi wa Mikopo NMB, Ally Ngingite (kushoto) ni Kamishna Mdaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zima Moto, Laizer Loshipay.
Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Aikansia Muro, (katikati) akimkabidhi sehemu ya Jezi za michezo, Mwenyekiti wa Kanda ya Ngome, Kanali Robert Mbuba, wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya Tsh. Milioni 16.7 kwa ajili ya timu za Majeshi zinazo shiriki michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) yanayotarajia kuanza mwezi wa Julai na Agost mwaka huu. (wa pili kulia) ni Meneja Mwandamizi wa Mikopo NMB, Ally Ngingite na Meneja Mwandamizi Idara ya Wateja Binafsi NMB, Isaac Mgwassa (kushoto) ni Kamishna Mdaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zima moto, Laizer Loshipay.
Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Aikansia Muro, (katikati) Mwenyekiti wa Kanda ya Ngome, Kanali Robert Mbuba, (wa pili kushoto) Meneja Mwandamizi wa Mikopo NMB, Ally Ngingite (wa pili kulia) eneja Mwandamizi Idara ya Wateja Binafsi NMB, Isaac Mgwassa (kulia) na Kamishna Mdaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zima moto, Laizer Loshipay, wakionesha sehemu ya Jezi za michezo baada ya makabidhiano ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya Tsh. milioni 16.7 wakati wa hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya Benki ya NMB jijini Dar es Salaam, leo Mei 7/2024 kwa ajili ya timu za Majeshi zinazo shiriki michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) yanayotarajia kuanza mwezi wa Julai na Agost mwaka huu.
Baadhi ya Viongozi wa Vioksi mbalimbali vya Majeshi waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya wafanyakazi wa NMB waliohudhuria hafla hiyo wakifuatilia kinachoendelea.

BENKI ya NMB imekabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh. Milioni 16.7, ambavyo ni sehemu ya udhamini kwa timu zitakazoshiriki Mashindano ya Baraza la Michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA), itakayofanyika Julai mwaka huu mjini Morogoro.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na jezi za mpira wa miguu 154, jezi za mpira wa kikapu pea 84, ‘tracksuit’ 32 na fulana ‘t-shirt’ 250, zitakazovaliwa na timu za Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Polisi, Zimamoto, Jeshi la Wananchi (JWTZ), Uhamiaji, Magereza na Idara Maalum za SMZ.

Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa NMB, Bi. Aikansia Muro, ndiye aliyekabidhi vifaa hivyo leo jijini Dar es Salaam kwa Kanali Robert Mbuba, aliyepokea kwa niaba ya Mwenyekiti wa BAMMATA, Brigedia General Saidi.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa pia na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Zimamoto na Uokoaji, Laizer Loshipay, Bi. Aikansia aliipongeza Kamati ya Mashindano ya BAMMATA kwa kuratibu na kusimamia michezo hiyo muhimu kwa Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

“Tunajisikia furaha kwa mara nyingine tena kuwa sehemu ya mashindano haya na tumekutana hapa kukabidhi vifaa mbalimbali ambavyo ni sehemu ya udhamini wetu kwa timu za majeshi yetu Tanzania Bara na Visiwani yanayoshiriki BAMMATA 2024.

“Kwa takribani miaka minne sasa, NMB tumekuwa tukidhamini michezo hii inayoratibiwa na BAMMATA na tunaamini ushirikiano huu wa muda mrefu utaendelea kuwa na manufaa kwa pande zote mbili kwa maana na NMB na Majeshi ya Ulinzi na Usalama.

“Kwa kutambua umuhimu wa michezo kwenye jamii na kwa kuthamini maudhuhi yanayobebwa na mashindano haya, tumeamua kutoa udhamini wa Sh. Milioni 16.7 kwa ajili ya kufanikisha mashindano ya mwaka huu mjini Morogoro,” alisema Bi. Aikansia.

Alibainisha kuwa NMB imekuwa ikidhamini michezo mbalimbali nchini, ambako kwa nyakati tofauti wamedhamini Taifa Stars, Azam FC, timu za mpira wa magongo pamoja, Kombe la Mkuu wa Majeshi la Gofu ‘CDF Trophy’ na mashirikiano na klabu za Simba na Yanga.

Kwa upande wake, Kanali Mbuba kwa niaba ya Kamati ya Utendaji ya BAMMATA, aliishukuru NMB kwa udhamini wao unaoenda kufanikisha mashindano hayo ya timu za Majeshi ambazo zitatumia vifaa hivyo kama chachu ya kufanya vizuri.

“BAMMATA tumefurahishwa na tukio hili, na ahadi yetu kwa Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya NMB ni kwamba tutaendelea kuwa wateja wa benki hii, ambayo imekuwa na huduma bora na rafiki kwetu na kwa jamii kwa ujumla.

“Kwa niaba ya Mwenyekiti wa BAMMATA, Brigedia General Saidi, tunaomba mashirikiano haya yawe endelevu na matarajio yetu ni kuona siku moja NMB inaingia mkataba wa kuwa Mdhamini Mkuu wa mashindano haya kwa miaka ijayo,” alisema Kanali Mbuba.

Mazungumzuzo yakiendelea kabla ya hafla hiyo kuanza.
Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Aikansia Muro, akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya Tsh. Milioni 16.7 kwa ajili ya timu za Majeshi zinazo shiriki michezo ya Majeshi Tanzania (BAMMATA) yanayotarajia kuanza mwezi wa Julai na Agost mwaka huu. (katikati) ni Mwenyekiti wa Kanda ya Ngome, Kanali Robert Mbuba na Kamishna Mdaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zima moto, Laizer Loshipay.
Afisa Habari wa NMB, Bethuer Kinyori,  akiendesha ratiba ya hafla hiyo
Mwenyekiti wa Kanda ya Ngome, Kanali Robert Mbubam akitoa shukrani zake kwa Benki ya NMB, baada ya kupokea vifaa vya michezo vyenye thamani ya Tsh milioni 16.7 kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Wateja Binafsi wa Benki ya NMB, Aikansia Muro, (wa pili yake) wakati wa wa hafla fupi ya kukabidhi vifaa vya michezo iliyofanyika Makao Makuu ya Benki hiyo jijini Dar es Salaam, leo Mei 7/2024. (wa pili kulia) ni Meneja Mwandamizi wa Mikopo NMB, Ally Ngingite na Meneja Mwandamizi Idara ya Wateja Binafsi NMB, Isaac Mgwassa 
Baadhi ya wadau na wafanyakazi wa NMB waliohudhuria hafla hiyo
Viongozi wakitambulishana kabla ya hafla hiyo kuanza.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.