Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Viongozi mbalimbali wakati wa Wimbo wa Taifa wa Kenya pamoja na ule wa Umoja wa Afrika (AU) ukiimbwa kabla ya kuanza Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuainisha vipaumbele vya Nchi hizo ili viweze kuzingatiwa kwenye mzunguko wa 21 wa IDA. Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB), alihudhuria mkutano huo. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi nchini Kenya
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB), akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El Maamry Mwamba, baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21), uliofanyika tarehe 29 Aprili mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi, Kenya.
Waziri wa Fedha Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (MB), akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Natu El Maamry Mwamba, na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Biashara Bi. Mary Kamari (kushoto), baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Uchangiaji wa Mzunguko wa 21 wa Mfuko wa Maendeleo wa Benki ya Dunia (IDA21), uliofanyika tarehe 29 Aprili mwaka huu katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta, Jijini Nairobi, Kenya.
.jpg)
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Nairobi-Kenya)
No comments:
Post a Comment